Tuesday, 27 February 2018

HUU NI UTAMADUNI WA AJABU NAMIBIA…..

Katika nchi ya Namibia kuna mambo mengi mazuri ya kuifanya nchi hiyo itembelewe na watu mbali mbali hasa kwenye swala la kuenzi na kuziendeleza tamaduni zao.

Ovahimba na Ovazimba kutoka pande za Kunene na Omusati wamekua wakiziendeleza tamaduni zao hasa kwenye kupokea wageni.
Katika jamii hiyo  wageni wakiume wanapowatembelea wanapewa walale na mke wa mmoja wa mwanafamilia, endapo kura za wengi zitaangukia kwake.
Mume huyo atapaswa aondoke chumba wanacholala na mke wake ili ampishe mgeni na kuhamia chumba kingine.
Iwapo wanakaa nyumba yenye  chumba kimoja itabidi  mwanaume akatafute sehemu nyingine akalale.

Mwanamke katika jamii hiyo anaweza kuwa na maamuzi madogo au kutokuwa na maamuzi kabisa, na endapo anarafiki zake inamlazimu awape kwa mume wake, japo haifanyiki mara nyingi. 

Reactions:

0 comments:

Post a Comment