This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Saturday, 28 April 2012

AJALI YA BASI LA COAST LINEHili ni basi la Coast line ambalo limepata ajali siku ya leo Juma mosi asubuhi katika kijiji cha Terrat kilichopo wilayani Sianjiro Mkoani Manyara.


Basi hilo lilikuwa likitokea Mkoani Arusha likieleke Mkoania Dodoma,na ndipo lilipopata na ajali hiyo katika eneo la kijiji hicho baaada ya STALING kukatika na kusababaisha kuugonga mti uliokuwa kando ya bara bara hiyo na kupelea tairi za mbele zote 2 kupasuka.


Basi hilo limeharibika vibaya sehemu ya mbele upande kulia ambao huwa anakuwa Dreva,amabaye amevunjika mguu mara mbili na abiria wengine kupata majeraha mbali mbali.           Hawa ni baadhi ya abiria walionusurika katika Ajali hiyoNa huu ndio mti wa Mgunga ambao Basi hili la COAST LIME limeugonga baada ya Kukatika STALING.

By Kiwa Strong..

Wednesday, 25 April 2012

KWA NINI VIUMBE WENGI WANA MACHO MAWILI

Nilikuwa natafakari juu ya uumbaji na kushangazwa na kitu kimoja cha ajabu; viumbe vingi hata vinavyoishi mazingira tofauti na vya aina (specie) tofauti sana vimefanana kwa kuwa na macho.


Vinaweza vyote visiwe na miguu, mbawa, au pua lakini karibu vyote vina macho. Kuanzia majini, angani na nchi kavu viumbe vingi vinamacho! Wadudu wadogo na wanyama wakubwa wote wana macho; samaki na ndege hadi minyoo ina macho! 

Na katika maajabu ndani ya maajabu ni kuwa viumbe vingi vina macho mawili (sijajua kama yupo mwenye jicho moja) na vile vingine vina macho mengi (compound eyes). Angalia mifano hii:

Angalia Nyoka:
Angalia Samaki:
Angalia Ndege:


Angalia Vipepeo


 


Angalia Mchwa

Angalia Nyangumi


Angalia Kaa:Angali Nyani:
Kwanini?
Jibu la kisayansi ambalo hutolewa mara nyingi ni "evolution"; lakini kwanini "eyes"? Utaona viumbe vinafanana vitu vingi tu lakini mara nyingi tofauti ni idadi.


kwa mfano viumbe vingi vina miguu minne (wanyama) lakini vipo vyenye miguu sita (wadudu) na vingine havina miguu kabisa (nyoka na samaki); lakini vyote vina macho! Kwanini macho ni mojawapo ya viungo ambavyo vinaonekana karibu katika viumbe vingi zaidi kuliko viungo vingine? Na kwanini mara karibu zote macho hayo yanakuwa mawili siyo matatu au manne (kuangalia pembeni, juu na chini)? 

Monday, 23 April 2012

NJIA KUMI KUSAIDIA KUPUNGUZA UNENE..

Kati ya sababu kuu zinazopunguza uhai wetu ni afya, unene na kutojua kujiangalia vyema.

 
1-ULAJI
Ipo mifumo miwili ya kula. Chakula unachokula na namna unavyokila.
Unavyokula.

Kuna kula vyakula vidogo vidogo vyenye madini, vitamini, mafuta nk mara nyingi kwa siku; au kula milo michache (mmoja au miwili) mikubwa ili kujaza tumbo. Ulaji mdogo mdogo husaidia afya na kuingia mwilini vyema kuliko ulaji mkubwa wa mara chache.

Tumbo lina musuli zinazofanya kazi kama mashine au mnyama. Gari likijaa sana hupata taabu kwenda. Punda hivyo hivyo. Ulaji mdogo mdogo unaosambazwa mara kadhaa kwa siku  ni bora maana mwili unachambua kila kitu kwa wepesi na haraka. Unapokula milo michache mikubwa unapalilia zaidi mafuta mwili.

(PENDEKEZO la kwanza.  Asubuhi, kunywa maji kwanza, matunda, kisha ndiyo chai na vitu vingine kama mkate au maandazi…)

Wapo wanaodai kwamba wanakula matunda na mboga...

Tatizo ni kwamba mipangilio  yao huwa ya makosa. Mathalan wengi hula matunda baada ya chakula. Vimeng’enya  chakula (enzymes) tumboni hufanya kazi namna tofauti. Mathalan vile vinavyonyambua matunda ni tofauti na vinavyomeng’enya vitu vigumu zaidi kama nyama au wanga.

Matunda hunyambuliwa haraka zaidi kuliko vyakula vingine. Hivyo ni bora kula matunda dakika10-20 kabla ya chakula. Ukila baadaye matunda hugeuzwa aina fulani ya pombe (fermented food) inayoelea tu juu ya chakula na kubakia kitu kingine badala ya kuingizwa haraka ndani ya damu kupitia utumbo mdogo, uwengu, moyo, ini, nk.

Tatizo jingine ni kupika sana mboga hadi zikapoteza nguvu.

Mseto wa vyakula pia ni muhimu. Kwa mfano vyakula vyenye uchachu (acid) na vile vinavyomumunyuka haraka (alkine) havitakiwi viliwe pamoja. Mfano ni matunda.

Matunda chachu kama machungwa, mananasi na maembe yatakiwa yawe pamoja; na yale laini zaidi:  ndizi mbivu, matikiti maji, mapapai, matufaha, nk yaende kivyake, maana yana mfumo tofauti, wa kumeng’enywa.

 

Chakula unachokula.....

Waafrika  hatuna tabia ya kula mboga mboga mbichi. Tunafuata ladha na mazoea kuliko thamani.
Bara letu lina mboga na vyakula bora kuliko bara lolote duniani lakini sisi tunakufa mapema na kwa utapia mlo kuliko wale wanaotoka nchi kame.

Ulaya nzima imejazana mboga mboga zinazoagizwa toka Afrika. Kenya na Tanzania zinauza mboga za maharagwe mabichi (green beans), matunda toka Afrika Kusini na Ivory Coast; nk. Waafrika tunapenda kujaza matumbo. Unene umekithiri hata wale walio matajiri waliosoma bado wanakufa kwa kisukari shauri ya kutokula mboga mbichi.

Ulaji wa mboga mbichi ni upi?

Ni mathalani ulaji wa salad. Tanzania tunaita kachumbari. Lakini si lazima iwe kachumbari ya nyanya, vitunguu na chumvi tu. Waweza kuchanganya matango, nyanya kwa maparachichi; au vitunguu saumu, giligilani na karote.

Huu mseto wa mboga mbichi ni mzuri ukienda na chakula chenye nyama za minofu na wanga (ugali, wali, ndizi za kupika nk). Ulaji wa wanga asubuhi, mchana na jioni kila siku huchangia sana katika unene.

2-UNYWAJI  MAJI
Waafrika hatunywi maji, hasa wanawake. Wanaokunywa maji zaidi ni wacheza michezo. Wengi wetu hunywa zaidi soda (vinywaji baridi kama Cocacola, Pepsi, Mirinda ,Tangawizi  na gesi za kisasa kama Red Bull) zilizojaa gesi inayoleta vidonda tumboni; na chai.

Kuliko maji. Na maji haya hutakiwa  dakika 10-20 kabla ya chakula au nusu saa kuendelea baada ya chakula. Ukila  chakula huku unasakatia maji huimanisha mtu una kiu.

Ulaji chakula na unywaji maji ni vitu viwili tofauti. Ila utawaona watu wanakula huku wakibugia maji. Unapokula chakula huku unabugia maji unapunguza nguvu za chakula, unajaza tumbo maji na kuchelewesha mmeng’enyo wa chakula (digestion).

Chakula kisipomeng’enywa vizuri kinaketi tu tumboni. Matokeo wengi wetu tuna  matumbo makubwa. Kama hufanyi mazoezi lile tumbo linakwenda pembeni (chini ya mbavu) hasa kwa watu wa makamo linaleta maradhi kama kisukari, kiungulia, kuvimbiwa, uyabisi wa tumbo, nk.


3-SUALA LA UMENG’ENYAJI

Chakula huanza kumeng’enywa au kusagwa (kwa lugha iliyozoeleka) mdomoni. Mate yako mdomoni ni chanzo cha uchambuaji chakula. Unapobugia chakula bila kutafuna sawasawa unasababisha mambo mawili.

Moja chakula kutochambuliwa vizuri, pili chakula kwenda kukaa tu tumboni, au kama kikipita hakisaidii lolote mwilini.

Utafunaji wa taratibu husaidia umeng’enyaji. Chakula kinapofika tumboni hukaa pale dakika ishirini. Hapo huchanganywa na asidi (ya manjano iitwayo Hydrochloric) inayokibadilisha tayari kupelekwa utumbo mkubwa, kupitia kongosho.

Kule uchafu utapelekwa chini na rutuba kusafirishwa na utumbo mdogo kuelekea katika uwengu, moyo. Moyo utadunda chakula kilichoshageuzwa damu kuelekea mwilini kufanya kazi na akiba hubakishwa katika ini.

Sasa kama usipotafuna vizuri, ukila huku unakunywa sana maji au vinywaji vingine chakula hakimeng’enywi vizuri. Ndiyo maana unawaona watu wengine wanakula sana lakini hawana afya.

Wanaugua ovyo ovyo, wanatoka jasho ovyo, wanajamba ovyo, wana matumbo makubwa, wanavimbiwa, wanakaa siku nyingi bila kwenda choo (inatakiwa mtu kwenda haja kubwa mara moja au mbili kwa siku) nk.

Misitu na hewa safi ya mimea

4-ULAJI WA VYAKULA VYA MAFUTA

Mafuta ni suala muhimu sana mwilini. Ila ulaji wake shurti uwe wa mpangilio. Yaani unaowiana. Lazima mtu uwe na wastani mzuri wa vyakula vya nguvu, yaani “wanga” (ugali, ndizi, wali, viazi mbalimbali, mikate, mahindi, nk), ujenzi yaani “protini” (mboga na nyama), “madini” (mbegu mbegu mbichi si za kukaanga sana na chumvi) na “vitamini” (matunda, maziwa, mayai, nk).

Waafrika tunapenda nyama. Nyama ni muhimu sana maana ina madini aina ya chuma (nyama nyekundu) protini,nguvu na mafuta. Ila mafuta yaliyoko katika nyama mara nyingi si mazuri shauri hayatoki, huganda.

Chukua nyama ya kuku na samaki ambayo huwa na ngozi. Wengi wetu hupenda sana kula ile ngozi ya wanyama hawa kwa kuwa tamu. Lakini haya ni mafuta mabaya.

Mafuta ya samaki lakini ni mazuri. Samaki anayo mafuta ya Omega-3 ambayo husaidia mwili na kinga maradhi mwilini.

Tunapokula nyama choma au ya kukaanga, lazima tule pia mboga za majani (mbichi) na si vizuri kula nyama kila siku. Kama huwezi kukaa bila nyama kila siku, fanya mazoezi ya mwili.

PENDEKEZO LA 3- Kula mbegu mbegu za korosho, karanga au mlozi (ziwe mbichi badala ya kukaanga na chumvi) kati kati ya siku. Haya ni mafuta yenye rutuba mwilini kuliko nyama za mafuta.


Chips za Magimbi

MAZOEZI YA MWILI NA VIUNGO

Mazoezi ni mfalme wa kupunguza unene.

Ukiwauliza wengi watakuambia wanafanya kazi ngumu za sulubu (wanachuruzikwa jasho) kwa hiyo hayo ni mazoezi. Ila kazi na mazoezi ni vitu viwili tofauti. Ingekuwa kufanya kazi ni mazoezi basi kusingekuwa na wastani mfupi wa maisha kwa maskini hasa sisi Waafrika.

Wengine watadai kwamba walipokuwa wadogo shuleni walifanya mazoezi sasa wamekuwa watu wazima (miaka 40 kuendelea) kwamba eti mazoezi ni suala la ujana; kumbe kadri unavyokuwa ki umri ndivyo kadri unavyotakiwa kufanya mazoezi na kujitazama zaidi kiafya.

Watazame Wachina na Wajapani wanavyoishi maisha marefu.

Mazoezi ni shughuli inayokufanya kwanza uheme (mapafu na moyo kwenda kasi), viungo na mifupa kujinyoosha (stretching), kutoka jasho na usafishaji wa damu.

Mazoezi yanayosaidia haya ni pamoja na kutembea kasi, kukimbia, kuogelea, michezo mbalimbali ya riadha (kama mpira wa miguu, nyavu, kikapu, mikono, nk); michezo ya kupigana na kujilinda yaani masho ati(karate, kung fu, judo, capoeira, krav maga, jiu jitsu, systema, kickboxing, thai boxing, kempo, kalari payatu, aikido, nk)

Ni muhimu mwanadamu ufanye mazoezi makali ya viungo mara mbili tatu kwa juma. Si vizuri kufanya kila siku kwani musuli na mishipa inahitaji kupumzika na kukua.

Kama unapenda kuinua vyuma lazima uwe na mwalimu wa kukuelekeza; na si vizuri kufanya kila siku.  Wastani wa mara mbili tatu kwa juma inatosha kabisa.

 

6-UPO UFANYAJI MAZOEZI WA AINA MBILI

Mazoezi ya nguvu ya kuhema niliyotaja hapo juu (cardio-vascular) na yale laini ya kujinyoosha yaani ambayo hutumia zaidi nguvu za ndani na pumzi.

Haya ya pili ni kama Yoga (India) , Tai Chi Chuan (China) na aina mpya mazoezi iliyoanza Majuu miaka ya karibuni yaani Pilates (hutamkwa hivyo hivyo ilivyoandikwa Pilates).

Haya laini yanawafaa zaidi watu wazima na nchini China na Japan mathalan utawakuta wazee wa miaka 80 hadi 90 bado wanayafanya. Husaidia moyo, damu na akili.

Michezo na mazoezi ya mwili ni njia kuu ya kupunguza unene, kurefusha maisha, kuchangamsha ubongo, kupunguza ulevi, uvutaji sigara, dawa za kulevya, tabia mbaya za uvivu, ugomvi, nk.  Mataifa yenye watu wanaofanya mazoezi kama Japan, Brazili, India, China nk  huwa na wachapa kazi wengi na wananchi wanaoipenda jamii yao.

Chakula cha wanga kwa wingi kilichozoeleka sana Afrika ni kitamu; ila kinakosa mboga mbichi za majani, yaani Saladi

7-KULA SANA CHUMVI SI VIZURI

Ulaji chumvi mwingi hutokana na suala la ladha. Kisayansi vyakula  vyote vina chumvi asilia sema tu tumezoea kuongezea madini hii iitwayo Sodium.

Sodium inachangia sana kufupisha maisha. Huifanya mishipa ya damu ichoke; ni kama bomba lolote la maji ukilitazama baadaye hugeuka rangi kutokana na yale maji kupita pale kila siku.

Kwa wale tunaoishi nchi za joto na kutoka sana jasho kula chumvi ni muhimu. Ila tatizo letu ni kwamba hatunywi maji ya kutosha.

Mtu ukiwa na kiu unakunywa soda au kinywaji cha sukari; inakuwa kama unaendelea kuutesa mwili.

Kwa vipi? Mishipa inayopitisha damu mwilini badala ya kusaidiwa kwa maji inawekewa kazi zaidi ya kusafisha sukari na chumvi. Ndiyo maana vifo vingi vinatokea mapema; wastani wetu wa maisha haupiti miaka 50.

Utafiti uliofanywa chuo kikuu cha California, Marekani mwanzoni mwa 2010, umethitibisha kwamba vifo vingi duniani husababishwa na maradhi ya moyo na saratani ambavyo hutokana na uvutaji sigara, unene, ulevi na ulaji sana wa chumvi na sukari.
Tukipunguza ulaji wa chumvi tunasaidia pia kupunguza maradhi ya moyo, utafiti unasema.


8-TAFITI ZA VYUO KADHAA ULIMWNGUNI KUHUSIANA NA AFYA

Jarida la Kimarekani la sayansi lilieleza kwamba utapunguza ugonjwa wa moyo (ambao husababishwa na unene , wasiwasi na purukshani) kwa asilia mia 42 kama utakula matunda na mboga za majani peke yake kila siku, juu ya msosi wa kawaida.

(PENDEKEZO LA KULA- Na 4- Kula mlo wako. Baada ya saa mbili au tatu, sakatia tunda au matunda; baada ya mlo mwingine, kula sahani ya mseto wa mboga mbichi kama karote na matango. Utaona tofauti ya afya, ngozi, wajihi,usingizi, nk.

Kidesturi tumezoea kunywa chai au soda za sukari sukari na gesi kati kati nya milo badala ya matunda na mboga mbichi za majani).

Utafiti uliofanywa na wanasayansi  chuo kikuu cha South Carolina mwanzo wa mwaka 2010 kuhusu faida za kuogelea.

-Zoezi la kuogelea  lina faida zaidi ya kukimbia au kutembea kwa vile huchanganya mazoezi makali na pumzi, kusaidia mapafu na moyo. Utafiti ulithibitisha kuogelea hupunguza hatari za kifo kwa asili mia hamsini.

-Utafiti wa jarida la chuo cha uganga Ulaya umeeleza (desemba 2009) kwamba kulala nusu saa kila mchana (“nap”) husaidia  kupunguza ugonjwa wa moyo kwa asilimia 37.

-Uchunguzi wa chuo cha michezo cha Hispania mwanzoni mwa 2010 umethibitisha kwamba ukikimbia mara tatu kwa juma (jogging) unaongeza nyege mwilini kwa asili mia 75. Hasa kwa watu wa makamo mnaoanza kupoteza nguvu za urijali.

-Uchunguzi chuo kikuu cha Leeds, Uingereza  mwanzoni mwa 2010 umeonyesha unapotembea kwa miguu, ukikwepa barabara kubwa zisisokuwa na mioshi ya magari (pollution) unapunguza matatizo ya maradhi ya hewa chafu kama pumu, mapafu na appendix.

-Uchunguzi wa chuo kikuu cha Texas mwaka 2010 umegundua kwamba  kula tunda la divai nyekundu mara kwa mara husaidia kupunguza  kupata ugonjwa wa kisukari.

-Hapo hapo tunaelezwa kwamba watu weusi na bara la Asia wanakumbwa zaidi na ugonjwa wa kisukari kutokana na vinywaji vya sukari sukari na gesi (fizzy drinks).

Ukinywa kiasi cha miligramu 300 za vinywaji hivi (Cocacola, Red Bull, Fanta, nk)  kwa siku unajitahadharisha kupata kisukari.

9-KUFUNGA

Neno kufunga linatambuliwa rasmi kuhusiana na Waislamu (mwezi Ramadhani) au Wakristo (Lenti nk). Ufungaji huo una masharti mengine ya kidini tofauti na haya ya kiafya.

Mathalani wafungaji  hawa hula chakula kingi usiku; ukihesabu wanafunga wastani wa saa 12 tu. Kawaida ukitaka virusi na takataka nyingine mwilini zitoweke, au viungo vipumzike wahitaji saa 20 kuendelea.

Ufungaji ninaouongelea ni ufungaji wa kutokula kabisa kwa saa 24, 36 hadi 48 kuendelea…
Ufungaji ni nini?

Kama mashine yeyote mwili wa mwanadamu unahitaji kupumzika na kujisafisha. Hata tukiwa tumelala bado viungo mbalimbali mwilini vinafanya kazi.

Kwa hiyo faida ya kwanza kabisa ya kufunga ni kuupumzisha mwili kama mfanyakazi yeyote anapokwenda likizo.

Faida ya pili ya kufunga ni kusafisha mwili kutokana na uchafu ambao haukutoka (kinyesi hakitoi mabaki yote toka utumbo mkubwa), dawa na takataka za mazingira tunayoyavutia hewa, virusi au kuyanywa katika maji na vyakula mbalimbali na pia uchafu wa hisia, yaani hasira, huzuni, nk.

Kuna ufungaji wa aina mbalimbali.

1-Kufunga kwa kunywa maji tu, saa 24 kuendelea…
2-Kufunga kwa kutokunywa maji au kula chochote, saa 24 kuendelea…
3-Kufunga kwa kula tu matunda au mboga zilizopondwa kama karote, matango nk, saa 24 kuendelea…

Ufungaji huu unatakiwa ufanywe kwa mpangilio. Kitu muhimu si tu kufunga bali NAMNA unavyofungua.

Ukianza kula tena, unaanza taratibu. Kawaida ni vizuri kuanza na maji, kikombe au bilauri ya kwanza taratibu.

Subiri tena nusu saa, bilauri nyingine, halafu hadi ya tatu, halafu ndiyo matunda yasiyo ya chachu, na kadhalika.

Kuanza kufungua kwa kunywa chai ya maziwa, uji au vyakula vingine vya wanga hakusadii sana mfungo huu.

Maana lengo lake ni kusafisha mwili.

10-USINGAJI

Usingaji au masaji ni njia nzuri sana ya kupunguza unene. Ikiwa unaangalia namna unavyokula, unafanya mazoezi na kusingwa mara moja au mbili kwa mwezi unaupalilia mwili vizuri.

Nini faida ya usingaji? Kusinga husaidia ngozi, mishipa ya damu na sura nzima ya mwili na taswira yako mwanadamu.

Wengi wetu tunaposikia neno kusinga tunafikiria usingaji wa mapenzi. Hivi ni vitu viwili tofauti kwani usingaji wa mapenzi unaimanisha mahusiano ya kihisia.

Kifupi mwanadamu unatakiwa uwe unautunza na kuungalia mwili wako kama nyumba au hekalu lako. Wengi wetu tunaoga, tunajipaka marashi, tunasuka, tunanyoa nywele au ndevu; lakini miili yetu kiundani inaoza taratibu…

By kiwa strong...........

Zijue faida za ajabu za kula karanga..!


Wengi wetu huchukulia ulaji wa karanga kama chakula cha kujiburudisha na kisichokuwa na umuhimu sana katika afya ya mwili wa binadamu. Kiukweli karanga siyo chakula cha kupuuziwa iwapo utajua faida zake kama nitakavyokujuza leo katika makala haya.

MAGONJWA YA MOYO....


Kama ilivyokuwa kwa korosho, karanga nazo ni chanzo kizuri cha mafuta mazuri aina ya ‘monounsaturated fats’ ambayo yanatiliwa mkazo kutumiwa kwa afya ya moyo. Kwa mujibu wa utafiti, watu wanaokula karanga mara kwa mara hupunguza hatari ya kupatwa na ugonjwa wa moyo (cardiovascular heart disease) kwa asilimia 21.

Aidha, katika taarifa iliyochapishwa kwenye jarida moja la Uingereza la ‘Journal of Nutrition’ ambako kuna matokeo ya taarifa nne za utafiti, imeonesha pia watu wanaotumia karanga mara kwa mara, angalau mara nne kwa wiki, hujipa kinga nyingine dhidi ya ugonjwa wa moyo (coronary heart disease) kwa zaidi ya asilimia 37.

Mbali ya kuwa na mafuta mazuri yanayotoa kinga kwenye moyo, karanga pia, hasa za kukaanga, zinaelezwa kuwa na kiwango kikubwa cha virutubisho vinavyotoa kinga ya mwili (antioxidants) kuliko hata kile kinachopatikana kwenye tunda la epo na karoti!

Ili kupata kinga hiyo dhidi ya aina hizo mbili za ugonjwa wa moyo, ambao unatesa watu wengi duniani na kugharimu pesa nyingi kwa matibabu, unashauriwa kula karanga pamoja na bidhaa zake kama vile ‘peanut butter’, angalau kijiko kimoja cha chakula, mara nne kwa wiki.

KINGA DHIDI YA KIHARUSI......


Ugonjwa mwingine hatari unaosumbua watu wengi hivi sasa ni kiharusi au ‘stroke’, lakini unaweza kujikinga nao kwa kuwa na mazoea ya kula karanga tu.

Utafiti umeonesha kuwa karanga ina kirutubisho aina ya ‘Resveratrol’ ambacho hupatikana pia kwenye zabibu na mvinyo mwekundu (red wine).

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa maabara na kuchapishwa kwenye jarida la Kilimo na Kemia ya Chakula (Journal of Agricultural Food Chemistry), umeonesha kuwa kirutubisho hicho huimarisha utembeaji wa damu kwenye mishipa inayokwenda kwenye ubongo kwa kiasi cha asilimia 30.

KINGA DHIDI YA KANSA YA TUMBO....


Faida nyingine inayoweza kupatikana kwenye mwili kutokana na ulaji wa karanga, ni kinga dhidi ya ugonjwa wa saratani ya tumbo.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa, unaonesha kuwa virutubisho vya ‘folic acid’, ‘phytosterols’, ‘phytic acid’ (inositol hexaphosphate) na resveratrol’ vinavyopatikana kwenye karanga, huweza kutoa kinga dhidi ya ugonjwa wa saratani ya tumbo.

Zaidi utafiti huo umeonesha kuwa ulaji wa karanga, hata mara mbili tu kwa wiki, una uwezo wa kupunguza uwezekano wa kupatwa na saratani ya tumbo kwa asilimia 58 kwa wanawake na asilimia 27 kwa wanaume!

Kwa maelezo hayo kuhusu faida za karanga mwilini, bila shaka chakula hiki kinapaswa kupewa kipaumbele katika orodha ya vyakula tunavyokula kila siku na hakika Mungu ametupenda sana kwa kutupa kinga dhidi ya maradhi yote yanayotukabili kwa njia ya vyakula.

By kiwa strong.....

HIZI HAPA HASARA NA FAIDA ZA KULA NYAMAKuna mjadala wa muda mrefu kuhusu suala la nyama nyekundu, ambapo makundi mawili tofauti yamekuwa yakitoleana hoja kuhusu faida na madhara ya kula nyama, hasa ile nyama iliyowekwa katika kundi la ‘nyama nyekundu’ (red meat).

Wakati wakereketwa wa masuala ya afya wanasema kuwa nyama nyekundu huchangia hatari ya mtu kupata ugonjwa wa moyo na saratani ya tumbo, wadau wa nyama wanadai kuwa hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya saratani, ugonjwa wa moyo na nyama nyekundu.

Wakereketwa wa masuala ya afya wanaeleza kuwa ukweli uko wazi kwamba nyama nyekundu inaweza kusababisha ugonjwa wa moyo kwa mtumiaji, kwani baadhi ya nyama nyekundu huwa na kiwango kikubwa mafuta (saturated fat) ambayo huongeza kolestro mwilini na mtu mwenye kiwango kikubwa cha kolestro huwa hatarini kupatwa na ugonjwa wa moyo.

Kwa upande wa saratani, watafiti wanasema kuwa bado hakujawa na ushahidi wa moja kwa moja kuwa nyama nyekundu inaweza kusababisha saratani ya tumbo. Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na Taasisi ya Afya ya Taifa nchini Marekani, umebaini kuwa watu wanaopenda kula kwa wingi nyama nyekundu, hufa mapema kuliko wale wanaokula kiasi kidogo cha nyama hiyo.

Wapenda nyama ambao wako kwenye hatari kubwa ya kupatwa na saratani na ugonjwa wa moyo ni wale wanaokula kuanzia kiasi cha gramu 112 za nyama (karibu robo kilo) kila siku, lakini wanaokula kiwango kidogo (nusu ya robo kilo) hawako hatarini na badala yake watapata virutubisho muhimu vinavyopatikana kwenye nyama.

Ulaji wa nyama nyekundu wenye faida kwa mwili wa binadamu ni ule unaozingatia kiasi na aina ya nyama. Nyama inayopendekezwa ni steki isiyo na chembe ya mafuta (lean meat) na itakayoliwa kwa kiasi kidogo.

Nyama inahitajika kiafya kwasababu ina madini ya chuma ambayo ni muhimu kwa wasichana na wanawake wanaotarajia kuzaa. Pia nyama ina Vitamini B12 ambayo husaidia utengenezaji wa DNA na hujenga mishipa na seli za damu. Halikadhalika kuna madini ya zinki ambayo husaidia kuimarisha ufanyaji kazi wa kinga ya mwili. Bila kusahau nyama ina protini ambayo ni muhimu kwa ujenzi wa mifupa na misuli.

JE, NGURUWE NI NYAMA NYEKUNDU?

Kumezuka swali pia kama nyama ya nguruwe nayo iko kwenye kundi la nyama nyekundu, kwani kimuonekano ni nyeupe.
Jibu ni kwamba nyama ya nguruwe nayo ni nyekundu.

Kwa mujibu wa Wizara ya Kilimo ya Marekani, kiwango cha protini aina ya ‘myoglobin’ kilichomo kwenye misuli ya nyama yoyote ndicho kinachoonesha aina ya nyama. Nyama ya nguruwe inahesabika kuwa ni nyekundu kwa sababu kiwango chake cha ‘myoglobin’ ni kikubwa kuliko kile kilichomo kwenye nyama nyeupe za kuku na samaki.

Kwa ujumla, nyama nyekundu ni muhimu kwa afya ya binadamu, lakini itakuwa muhimu kama itatumiwa kwa kiwango na kiasi kinachotakiwa. Siku zote epuka kula nyama yenye mafuta na badala yake pendelea kula steki isiyokuwa na mafuta ili upate virutubisho vyake muhimu kwa afya yako.

Kula nyama kinyume na mwongozo huu, ni sawa na kuamua kujiweka katika hatari ya kupatwa na ugonjwa wa moyo na matatizo mengine ya kiafya, ikiwemo ugonjwa wa miguu au kansa ya tumbo. Jiepushe na hayo kwa kuzingatia masharti ya ulaji sahihi.
By kiwa strong..

Wednesday, 18 April 2012

Tambua madhara ya kunywa Soda
Kuna mjadala mkali unaendelea kuhusu vinywaji baridi hususani soda, baada ya utafiti wa hivi karibuni kuonyesha kuwa soda inaweza kuwa na madhara zaidi kiafya kuliko hata sigara!

Hii inaweza kuwa changamoto nyingine kubwa kumkabili binadamu katika masuala ya afya, kwani makampuni makubwa yanayotengeneza vinywaji baridi yanatumia mabilioni ya dola kila mwaka,kujitangaza na kutoa misaada ya kijamii kutokana na mauzo yake bila kutaja madhara ya vinywaji vyao.

Soda inahusishwa na matatizo mengi ya kiafya kwa watoto na watu wazima, yakiwemo matatizo ya kuongezeka unene kupita kiasi (obesity), ugonjwa wa ini (liver disease) na hata tabia za vurugu (violent behavior).Kwa mujibu wa utafiti wa hivi karibuni, unywaji wa vinywaji baridi mara kwa mara unachangia tabia ya ugomvi kwa asilimia kati 9-15!

Kwa mujibu wa utafiti huo uliofanywa nchini Marekani, soda huwekwa ‘fructose’ (sukari) nyingi ikiwa katika mfumo wa sirapu (fructose corn syrup) ambayo inaongoza kwa kusababisha magonjwa ya unene, kisukari, ugonjwa wa moyo na magonjwa mengine sugu yanayowakabili Wamarekani wengi hivi sasa na dunia kwa ujumla.

Dk. Mercola, ambaye ni mtaalamu wa masuala ya lishe asilia na tiba mbadala anasema: ” Ninaposema kunywa soda ni hatari sawa na mtu anayevuta sigara au pengine zaidi, siyo jambo la kutia chumvi, bali ndiyo ukweli halisi”.

Dk. anaendelea kusema kuwa unywaji wa soda kwa njia nyingi ni mbaya kuliko uvutaji wa sigara, ila kutokana na kampeni kubwa ya matangazo inayofanywa na makampuni haya, inafanya vinywaji hivi vyenye sukari kuonekana havina madhara kwa watu wasio na hatia, hasa watoto wetu!

SABABU KUBWA YA KUDHARAU SODA:


Bila shaka utakuwa unashangaa na kujiuliza soda ina ubaya gani? Kwa mujibu wa Dk. Mercola, hakuna sababu yoyote ya kuendelea kunywa soda, labda ujikute uko katikati ya jangwa na haku
na kinywaji kingine isipokua soda!

Kiafya unywaji wa soda au vinywaji vingine baridi vyenye ‘fructose’(sukari nyingi) una madhara.Unywaji wa kiasi cha kopo moja tu la soda kila siku, utakuongezea uzito wa mwili wa kilo 10 kila mwaka na hatari ya kupatwa na ugonjwa wa kisukari (diabetes) kwa asilimia 85!

FRUCTOSE:Ni kirutubisho kilichomo ndani ya sukari na kiwango kinachowekwa wakati wa utengenezaji wa soda ni kingi kuliko kawaida.


Inaelezwa kuwa miaka 100 iliyopita, Mmarekani mmoja alikuwa akitumia kiasi cha gramu 15 ya sukari (fructose) kwa siku, tena kwa kula matunda.


Miaka 100 baadaye, (yaani hivi sasa), robo ya Wamarekani wote wanatumia kiasi cha gramu 135 (kutoka 15) kwa siku tena kwa kunywa soda!

Ulaji wa sukari (fructose) kiasi cha gramu 15 kwa siku hauna madhara kiafya, labda uwe na ugonjwa wa kisukari (high uric acid levels).Hata hivyo kwa kula sukari mara kumi zaidi ya kiwango cha gramu 15 kinachokubalika kiafya, inakuwa ndiyo chanzo cha unene wa kupindukia na magonjwa mengine hatari yanayoibuka mwilini (degenerative diseases).


Utafiti unaonesha kuwa vinywaji vingi baridi vina sukari nyingi kuliko wastani unaotakiwa.Badala ya kuwa na asilimia 55 ya ‘fructose’ na asilimia 45 ya ‘glucose’, vingi vina asilimia 65 ya ‘fructose’, ikiwa ni karibu asilimia 20 zaidi na inavyotakiwa.

Utafiti zaidi umeonesha kuwa ‘fructose’ ndiyo chanzo kikubwa cha tatizo la ugonjwa wa ini kwa watoto wengi nchini Marekani, ingawa hawatumii kilevi chochote (alcohol).Inaelezwa kuwa ‘fructose’ huleta madhara kwenye ini kama inavyofanya pombe.


N:B


Kama ulikuwa hujui kwa taarifa yako ni kwamba kwenye chupa moja ya soda kuna vijiko 10 vikubwa vya sukari.....


Kazi ni kwakoo kuamua kunywa sodaa au kuachaaaaaaaa sasaaaaaaa...


By kiwa strong...

Uvutaji wa sigara katika ndoa:

Wake au waume wa wanandoa ambao wanavuta sigara wamekuwa na wakati mgumu sana katika hisia zao,hasa kutokana na tabia ya kuvuta sigara kwa hao partners wao.

Hisia huweza kuwa ni za hofu, mashaka na kujisikia kutothaminiwa au kuwa disappointed na hata kuumizwa na hiyo tabia.Wapo partners ambao hutafsiri kwamba kitendo cha kutoacha kuvuta sigara,ni kuonesha kutojali afya yake mvutaji na familia kwa ujumla yaani mke, mume na watoto.


Anyway kila mvutaji hupenda kuacha kuvuta sigara hata hivyo hamu na uhitaji wa kuvuta sigara huwa kubwa zaidi,kuliko makali ya kifo hii ina maana mvuta sigara akiwa na hamu ya sigara huwa radhi kukubali kuvuta sigara kuliko kutovuta kwa kuogopa kifo.


Ukishajiingiza kwenye kuvuta sigara na kuwa addicted na nicotine iliyomo katika Sigara,utakuwa radhi kukubali kifo kuliko kuacha kuvuta.


Kumbuka:

Wavuta sigara huwa na magonjwa mengi kuliko wasiovuta,pia wavuta sigara huishi muda mfupi kuliko wasiovuta.

Ukivuta sigara kwa zaidi ya miaka 30 unaweza kuwa umetumia pesa yenye thamani ya zaidi ya TSh. millioni 200.By Kiwa strong

Tuesday, 17 April 2012

Faida ya ndizi mbivu katika mwili wa binadamu


Ni kinga dhidi ya magonjwa ya moyo, presha, vidonda vya tumbo, saratani ya figo, kukosa choo

Ndizi mbivu ni tunda ambalo linafahamika na kila mtu, lakini sina hakika kama watu wengi wanafahamu umuhimu na faida za tunda hili ambalo linapatikana kirahisi sana nchini. Bei yake ni kati ya shilingi 50 na 150 tu, kiwango cha pesa ambacho kila mtu anaweza kukimudu.

Iwapo ulikuwa hujui umuhimu wa kula ndizi mbivu, leo utalazimika kubadili mtizamo wako na kuziangalia ndizi kama tunda muhimu katika kuupa nguvu na kuulinda mwili wako dhidi ya maradhi hatari ambayo hayana tiba. Watu wa michezo pia wanapaswa kuliona tunda hili kuwa ni muhimu sana katika kuipa miili yao nguvu.

KINGA DHIDI YA SHINIKIZO LA DAMU NA MARADHI YA MOYO

Kwa mujibu wa utafiti wa kisayansi, ndizi ni chanzo kikubwa cha Potassium, madini ambayo ni muhimu sana katika kuweka shinikizo la damu mwilini katika hali yake ya kawaida (Normal Blood Pressure), na ufanyaji kazi mzuri wa moyo. Kwa kuwa ndizi moja ina wastani wa 467mg za madini aina ya Potasiamu na 1mg ya sodiamu (chumvi), ndizi moja tu kwa siku inaweza kukupa kinga ya maradhi ya shinikizo la damu na matatizo ya moyo.

Ukweli kuhusu vyakula vyenye kiwango kikubwa cha madini ya Potasiamu katika kushusha shinikizo la damu mwilini, umethibitishwa na tafiti nyingi za kisayansi. Kwa mujibu wa jarida moja la masuala ya afya nchini Marekani, zaidi ya Wamarekani 40,000 wa kike na kiume, walifanyiwa utafiti kwa muda wa miaka minne na ikagundulika kwamba watu wanaokula vyakula vyenye kiasi kikubwa cha madini ya Potasiamu na kirutubisho cha Fiber (Ufumwele), wako katika hatari ndogo ya kupatwa na kiharusi.

Aidha, utafiti mwingine uliofanywa na taasisi moja ya masuala ya tiba ijulikanayo kama Archives of Internal Medicine, ya nchini Marekani, pia ilithibitisha kwamba ulaji wa vyakula vyenye kiasi kikubwa cha ufumwele (fiber) kama vile ndizi, husaidia sana kutoa kinga dhidi ya maradhi ya moyo. Na katika suala hili, zaidi ya watu 10,000 walifanyiwa utafiti kwa muda wa miaka 19.

KINGA DHIDI Y VIDONDA VYA TUMBO

Kwa muda mrefu sana imethibitishwa kwamba ndizi ina virutubisho vyenye uwezo wa kupambana na asidi tumboni hivyo kutoa kinga dhidi ya vidonda vya tumbo (stomach Ulsers) na kutoa ahueni kwa mtu ambaye tayari ameathirika. Katika utafiti mmoja, ilkibainika kwamba mtu akila mchangayiko wa ndizi mbivu na maziwa freshi, huzuia utokaji wa asidi tumboni inayosababisha vidonda vya tumbo.

Kwa mujibu wa utafiti wa kisayansi juu ya suala hili, ndizi hutoa kinga na ahueni ya vidonda vya tumbo kwa njia mbili. Mosi: virutubisho vilivyomo kwenye ndizi huzipa uhai seli zenye kazi ya kutengeneza utandu ambao hutoa aina fulani ya urojo (mucus) unaotumika kama kizuizi dhidi ya asidi tumboni.

Pili: kuna virutubisho vingine kwenye ndizi ambavyo kwa kitaalamu vinajulikana kama ‘Protease’ ambavyo husaidia kuondoa bakteria tumboni ambao wanaelezewa kuwa ndiyo chanzo cha vidonda vya tumbo. Hivyo kama wewe hujaptwa na vidonda vya tumbo, kwa kula ndizi mara kwa mara unajipa kinga madhubuti na kama tayari umeathirika na vidonda, kwa kula ndizi utajipa ahueni kubwa.

NDIZI KAMA TIBA KWA WENYE MATATIZO YA CHOO

Ndizi ni muhimu sana katika kulainisha na kusafisha tumbo na kumuwezesha mtu kupata choo. Mbali ya kusaidia upatikanaji wa choo kwa wenye matatizo hayo, lakini pia hutoa ahueni kwa wagonjwa wa kipindupindu. Mtu aliyepatwa na kipindupindu hupoteza kiasi kikubwa cha madini ya Potasiamu, hivyo kwa kula ndizi ataweza kurejesha mwilini maidni yake yaliyopotea na kuupa mwili nguvu yake.

UIMARISHAJI WA NURU YA MACHO

Wakati ulipokuwa mdogo, bila shaka uliwahi kuambiwa na mama kuwa mtu akila karoti, atakuwa akiona vizuri. Bila shaka hakukosea, lakini sasa ukiwa mtu mzima unaambiwa kwamba ulaji wa matunda, ikiwemo ndizi, ndiyo kinga hasa dhidi ya matatizo ya kutokuona vizuri uzeeni. Utafiti wa hivi karibuni unaonesha kwamba ulaji wa matunda kwa wingi kila siku, hupunguza kwa asilimia 36 matatizo ya kutokuona vizuri kutokana na mtu kuwa na umri mkubwa.

KINGA DHIDI YA SARATANI YA FIGO

Utafiti wa hivi karibuni uliochapishwa na Jarida la Kimataifa la masuala ya Saratani (International Journal of Cancer) la nchini Marekani, umeonesha kwamba ulaji wa mara kwa mara wa matunda halisi, hasa ndizi mbivu, ni kinga madhubuti ya mwili. Zaidi ya wawake 50,000 wenye umri kati ya miaka 40 na 76 waliofanyiwa utafiti, ulionesha kuwa wale waliokula wastani wa milo 2.5 ya matunda na mboga kila siku, walipunguza hatari ya kupatwa na saratani ya figo kwa asilimia 40.

Baadhi ya vitamini na madini yaliyomo kwenye ndizi ni pamoja na Vitamini B6, Vitamin C, Potassium, Dietary Fibre na Mnganese. Hivyo utaona kwamba tunda la ndizi ni muhimu kwa sababu limesheheni vitamini na madini muhimu katika mwili wa binadamu. Kuanzia leo itazame ndizi kama tunda muhimu sana katika ustawi wa afya yako na ni kinga dhidi ya maradhi unayoweza kuyaepuka kesho kwa kula tunda hili kwa wingi leoBy kiwa Strong.. Umuhimu wa matumizi ya chumvi kwa Binadamu

CHUMVI ni aina ya madini yenye umuhimu na faida nyingi, kwa mtumiaji, ikiwa atatumia kwa kiasi kinachotakiwa kwenye mlo wake. 

Kwa maisha ya kawaida, huwezi kukosa madini hayo au kiungo hicho kwenye familia mbalimbali, mara nyingi utaikuta jikoni au hata mezani. Chumvi pamoja na muonekano 
wake ni kiungo au madini ambayo hupatikana kwa urahisi na bei nafuu kuliko viungo vingine vya chakula au madini duniani. 

Pamoja na umuhimu wake, lakini si rahisi ukasikia kesi au masuala ya chumvi kuibwa kama zilivyo bidhaa nyingine kwenye maduka mbalimbali. Mfano mdogo ni kiungo kama mafuta ya kula, hiyo ni bidhaa ambayo ukiiweka pamoja na chumvi, ukamwambia mtu achague bidhaa 
moja aondoke nayo, wengi watachagua mafuta. 

Lakini jamii inapaswa kufahamu kwamba, katika afya ya mwanadamu au hata mnyama chumvi ina umuhimu mkubwa, ingawa wengi wetu tunaona ni kiungo cha kawaida sana. Ni miaka mingi sasa chumvi (chloride), inatumika kuhifadhi vyakula, kuongeza ladha kwenye chakula na mara nyingine hutumika kusafisha vitu. 

Kwa kawaida chumvi ni madini au tunaweza kuita rasilimali isiyoisha, ambayo hupatikana kwa urahisi na ili ifae kwa matumizi ya binadamu huhitaji kuongezwa madini joto. 

Chumvi huzalishwa kwa njia mbalimbali, kuna chumvi iliyotengenezwa mahususi kwa ajili ya matumizi ya jikoni, mezani na pia ipo chumvi iliyoongezwa madini ya chuma ambayo ndiyo inayotumika kwa wingi katika jamii. 

Kwa wale wasiofahamu manufaa ya chumvi na matumizi yake ni vyema wafahamu na kuchukua hatua kwani matumizi ya chumvi pia ni tiba kwa baadhi ya maradhi na pia hupunguza kero zitokanazo na kuumwa na wadudu mbalimbali. 

Kwa matumizi jikoni Mbali na kutumika kwenye maabara kwa kuhifadhi vyakula, kuoka, chumvi hutumika jikoni kwa kuongeza ladha kwenye vyakula mbalimbali vipikwavyo. 
Pia chumvi hutumika kuchunguza iwapo mayai ya kuku au bata kama ni mabovu au mazima. 

Katika upimaji huo, tumia kijiko cha chai kupima, ambapo weka chumvi vijiko viwili, changanya na maji kwenye bakuli au chombo, kisha tumbukiza yai moja baada ya jingine. 

Ikiwa yai ni bovu litaelea juu ya maji na kama ni bovu au lina muda mrefu tangu litagwe na kuku au bata litazama kwa kuwa kiwango cha hewa ndani ya seli ya yai huongezeka kadri yai linapokaa muda mrefu baada ya kutagwa. 

Hata hivyo kama yai limeelea huenda sio bovu ila limekaa muda mrefu baada ya kutagwa na njia muafaka wa kubaini baada ya kulipima kwa njia ya chumvi ni kulipasua na kuona ndani kuna nini. Kadhalika yai kama ni zima litazama hadi chini kwenye chombo husika. 

Kuhifadhi matunda yasiharibike rangi Matunda mengi duniani kama vile tufaa na peas huhifadhiwa kwa kutumia limau au siki kufanya matunda hayo yasibadilike rangi na kuwa ya udhurungi au kahawia. 

Lakini chumvi nayo hutumika kwenye kazi hiyohiyo kwani sio wote wenye uwezo wa kununua siki au malimau ya kutosha kuhifadhi matunda, ila kiasi kidogo tu cha chumvi kilichochanganywa na maji hufanya matunda kuwa katika rangi yake ya kawaida kwa muda mrefu. 

Usafi wa kinywa Chumvi hutumika pia kufanya mswaki wako udumu muda mrefu. Kabla ya kutumia mswaki mpya chukua kiasi kidogo cha chumvi changanya na maji kisha tumbukiza mswaki kwa muda kidogo halafu utoe. 

Njia hiyo hufanya mswaki kudumu muda mrefu bila kuharibika, kukakamaa au kutengeneza umbo kama ua lililochanua. Kadhalika chumvi hutumika kusafisha meno, ambapo kiasi kidogo 
cha chumvi huwekwa kwenye mswaki na mtumiaji kuswaki ambapo matokeo yake meno hung’aa na kuwa imara. 

Wataalamu wa afya ya kinywa wanasema chumvi ni nzuri pia kwa kutunza kinywa dhidi ya harufu mbaya. Katika jamii wapo baadhi ya watu ambao midomo yao hutoa harufu. Ili kuzuia kero hiyo kiasi cha chumvi pamoja na maji ya uvuguvugu mtumiaji husukutua kinywa na hatimaye kuondoa harufu hiyo mbaya. 

Kuumwa na wadudu Watabibu wanasema chumvi hutumika pia kutibu au kupunguza makali 
ya kuumwa na wadudu kama vile nyuki na wadudu watambaao. Utafiti wa sayansi mbalimbali katika vyuo vya tiba na dawa nchini Marekani, na Uingereza wanasema kiasi cha chumvi husaidia kupunguza maumivu ya kuumwa na nyuki au wadudu wengine. 

Kiasi kidogo cha chumvi huwekwa kwenye eneo lililoumwa na nyuki au wadudu na baada ya muda kidogo, maumivu hupungua kama sio kuisha. Pia kuna baadhi ya watu wakiumwa na mbu hubakia na vipele ambavyo vina maumivu, hivyo wataalamu wanashauri kwamba kiasi cha chumvi kilichochanganywa na mafuta ya mzeituni kitumike kutibu eneo hilo. 

Kadhalika magonjwa ya koo kama vile muwasho wa mafua kiasi cha chumvi ilichochanganywa na maji ya uvuguvugu, mgonjwa akitumia kusukutua, huleta nafuu kwa mgonjwa. Chumvi hutumika pia kufukuza wadudu kama vile sisimizi na siafu nyumbani. 

Kwa wapambaji kwenye maeneo mbalimbali kama vile kumbi za harusi na hata nyumbani, chumvi hutumika kufanya maua yadumu kwa muda mrefu bila kunyauka. Chumvi kiasi huchanganywa kwenye maji katika chombo cha maua na kisha kutumbukiza maua, ambayo 
yatadumu kwa muda mrefu bila kunyauka. 

Hayo ni baadhi tu ya matumizi ya chumvi kiafya na pia katika matumizi mengine, wataalamu wa afya wanashauri kwamba kiasi cha chumvi mwilini ni muhimu kwa afya na uhai wa binadamu. Hata hivyo wataalamu wa afya wanashauri kwamba chumvi itumike vizuri kwani itumikapo vibaya huwa na madhara mbalimbali. 

Madhara hayo hutokana na jinsi chumvi hiyo ilivyotayarishwa yaani kutoka kuchimbwa ardhini hadi kufungashwa tayari kwenda kwa mlaji. 

Mtu akipatwa na shinikizo la damu ana uwezekano mkubwa wa kuwa na magonjwa ya moyo, ambayo ni pamoja na moyo kushindwa kusukuma damu na mengineyo ambayo huweza kusababisha mtu akapatwa na mshtuko wa ghafla wa moyo na kisha akapoteza maisha. 

Jambo hilo limegunduliwa na Watafiti wa masuala ya afya wa vyuo mbalimbali duniani wakiwemo wa Chuo Kikuu cha California, Marekani. Imebaikina kwamba kwa kila binadamu wenye umri mkubwa watatu, mmoja kati yao anasumbuliwa na shinikizo la damu. 

Ushauri wa kitiba unasema ni vyema wanadamu wakapunguza matumizi ya chumvi yasiyo na lazima kwenye vyakula. Inashauriwa kwamba kwa siku moja kiasi cha miligramu 2,400 cha 
chumvi ndicho kinahitajika mwilini na si zaidi. 

Kiasi hicho ni sawa na kijiko cha chai kimoja, na kwa wale wenye tatizo la shinikizo la damu kiasi cha miligramu 1,500 sawa na nusu kijiko cha chai cha chumvi. Mtafiti katika chuo hicho, 
Dk.Kirsten Bibbins-Domingo anasisitiza matumizi sahihi ya chumvi kiasi kwa ajili ya kupunguza uwezekano wa kupata maradhi yanayotokana na shinikizo la damu. 

Kwa wale wanaopenda kula vyakula vilivyokwisha fungashwa ni vyema wakasoma maelekezo na kuona kiasi cha chumvi kilichowekwa, ili kuepuka matumizi mengi ya madini hayo mwilini. 
Anasema chumvi ikitumiwa kwa kiasi haina madhara na pia ni dawa, lakini matumizi mabaya ya madini hayo huleta madhara makubwa kwa afya wa walaji, pasipo wao kufahamu. 

Katika matokeo ya utafiti mmoja kuhusu matumizi ya chumvi kwa binadamu, wanasayansi wa tiba wamebaini kwamba matumizi madogo ya chumvi hupunguza hatari ya kupata magonjwa ya mishipa ya moyo. 

Kila mwaka magonjwa mapya ya moyo zaidi ya 120,000 hujitokeza, wanaopata kiharusi wakiwa zaidi ya 67,000 na mshuko wa moyo wagonjwa zaidi ya 100,000. Wagonjwa hao ni katika pembe mbalimbali za dunia na kwamba matumizi sahihi ya chumvi kwa waliozingatia yamesaidia kupunguza tatizo hilo kwa Bara la Afrika na Amerika. 

Matumizi hayo sahihi wa watu wa mabara hayo mawili yamesaidia kuzuia vifo takribani 92,000 kwa mwaka.

JIWE LA MSINGI LA KWANZA=KIWA                KIWA STRONG- Knowledge Inteligent With Action=KIWA


Katika maisha siku zote ni kutokukata tamaa katika jambo unalolifanya,hiyo ndiyo siri ya mafanikio sababu yoyote unayemwona ana mafanikio basi kuna vikwazo amevipitia lakini hakukata tamaa.


Na wewe pia hali uliyonayo  ni zamu yako kuonyesha ujasiri wako juu ya mikwamo unayokutana nayo katika maisha.
Sababu ya kupoteza Nywele-Kichwani a.k.a UPARA


Causes Of Hair Loss
Tafiti kusema kwamba moja ya mambo ya kwamba kufanya watu kupoteza imani yao ni kupoteza nywele. Hii ni kwa sababu watu wengi hawawezi kuwa na uhakika mbele na hata karibu na watu wengine kujua kuwa watu hawa ni wazi staring katika matangazo yake bald.
Wataalam wanasema kwamba nywele hasara au upaa inaweza kuepukika kwa watu hasa kama familia zao na historia yake. Watu hawa, jeni ambaye alifika kutoka vizazi wakubwa ambao ni kukabiliwa na kupoteza nywele, kweli hawezi kufanya mengi kuhusu hilo tangu hali anaendesha katika jeni yao. Lakini kwawale ambao hawana katika jeni yao na bado kupoteza sana nywele, sasa ni wakati wa kuwa na wasiwasi.
Ni nini sababu ya kupotea kwa nywele?
Zaidi na zaidi ya watu ni kuwa kukabiliwa na kupoteza nywele kwa sababu hawana kulipa kipaumbele kwa ishara na dalili za hali. Ikiwa ni kukabiliwa na upaa, Jambo la kwanza kwamba unahitaji kuangalia, mbali na historia ya familia ya kupoteza nywele, ni idadi ya kuachwa ya kupoteza nywele kwamba katika siku.
Ingawa ni vigumu kabisa kuweka wimbo wa idadi halisi ya kuachwa, mia kuwa liko kama haionyeshi kwa karibu. Wataalam wanasema kwamba hii kiasi cha kupoteza nywele ni kawaida kwa sababu anasimama mpya ya nywele inatarajiwa kuongezeka katika 12 wiki. Lakini kama kiasi ni zaidi ya hii, ni lazima kuzingatia inaweza kusababisha.
zifuatazo ni baadhi ya sababu ya kawaida ya kupoteza nywele. Ingawa baadhi ya ambayo inaweza binafsi ya kuamua, daima ni bora kwa shauriana na mtaalam kwa sababu anaweza pinpoint nini hasa sababu upaa wako.
1. Magonjwa, magonjwa na wengine hali ya matibabu.
Hii ni moja ya sababu ya kawaida ya kupoteza nywele. Magonjwa kama vile ugonjwa wa kisukari, lupus, au wale kwamba ni kuhusishwa na tezi thioridi unaweza kuathiri ukuaji na uzalishaji wa jumla wa nywele katika mfumo wa mtu.
2. Kuchukua dawa fulani.
madhara ya madawa fulani kama ya isotretinoin na lithiamu chakula na dawa nyingine ambazo zina amfetamin zinajulikana kusababisha kupotea kwa nywele hasa miongoni mwa vijana. Watu ambao wanaendelea na vikao vya kutibu saratani ya kidini pamoja na madawa hayo kwa gout, unyogovu,arthritis, na matatizo ya moyo inaweza kusababisha upaa. Katika wanawake, kuzaliwa kudhibiti dawa pia inaweza culprit kwa hasara nywele.
3. Utapiamlo au lishe duni.
Watu walio na upungufu wa protini na chuma katika miili yao uwezekano wengi wanakabiliwa na kupoteza nywele. Hii ni kwa sababu hizi mbili ni sehemu muhimu kwamba nywele nguvu ya kufanya hivyo kukua. Nywele hasara kutokana na lishe mbaya ni zaidi miongoni mwa wanawake kwa sababu wao ni wale ambao ni zaidi ndani ya fad na mlo ambayo kusababisha matatizo ya kula kwamba sababu chini ya lishe. Wataalam wanasema kwamba wakati mtu ana lishe duni, kuna kutosha ugavi wa virutubisho kama vile vitamini na madini na kuendeleza ukuaji wa nywele.
4. Wanaendelea na matibabu ya matibabu.
Watu walio na kufanyiwa matibabu ya matibabu kama vile kidini na mionzi ya Mambo ya Msingi ni kupata zaidi katika hatari ya kupoteza nywele zao kwa sababu hizi matibabu inaweza kuua nywele kutoka mizizi na huweza hata kusababisha hali inayoitwa “alopecia” ambayo inaweza kusababisha hasara ya kudumu nywele.
Sababu nyingine ya kupoteza nywele ni pamoja na mabadiliko ya homoni, nywele matibabu na hairstyling, kichwani maambukizi, “trichotillomania” au nywele-kuunganisha machafuko, na kuvuruga mzunguko wa ukuaji wa nywele.