Kifafa cha
mimba ni ugonjwa
unaowapata wanawake wajawazito, hasa wenye mimba za kwanza.
Kwa walio wengi, ugonjwa huu hutokana na kupanda kwa msukumo wa
damu (High blood pressure). Ugonjwa huu utokeapo, mgonjwa hupatwa na degedege
(convulsions).
Kifafa cha uzazi au wengine wanakiita kifafa cha mimba ni
miongoni mwa matatizo yanayosababisha
vifo vya wajawazito nchini.
Kifafa cha mimba kinaweza kutokea wakati wa ujauzito, wakati wa
kujifungua au baada
ya kujifungua
ya kujifungua
Matibabu ya kifafa cha mimba
Tiba pekee ya kifafa cha mimba ni kumzalisha mjamzito. Hii ni
kwa sababu ugonjwa huu husababishwa na kuwepo kwa kondo la nyumba ndani ya
kifuko cha uzazi. Bila kutoa kondo la nyuma mgonjwa hawezi kupona.
Iwapo ugonjwa huu utagundulika kabla mtoto hajakomaa na kuwa
tayari kwa kuzalishwa.
Daktari anaweza kushauri mjamzito alazwe na kuangaliwa kwa
ukaribu wakati ikisubiriwa kukomaa kwa mtoto. Vilevile daktari anaweza kushauri
mjamzito apewe dawa ya kuharakisha kukomaa mapafu ya mtoto.
Iwapo hali ya mjamzito ikibadilika na kuwa mbaya, kumzalisha
itakuwa ni lazima hata kama mtoto hajakomaa kwa sababu kuna hatari kubwa ya
mama na mtoto kuathirika iwapo ujauzito utaendelea kuwepo.
Mojawapo ya hatari inayoweza kutokea iwapo ujauzito utaachwa ni
mtoto kufia tumboni, kupoteza fahamu kwa mjamzito na kupata dalili za
“degedege“.
Pia mgonjwa anaweza kupoteza uwezo wa damu pamoja
kuganda jambo ambalo husababisha mjamzito kupoteza damu nyingi.
Damu inapoganda mwilini na kuziba mishipa, kondo la
nyuma hujitenga na kifuko cha uzazi kabla ya mtoto kuzaliwa pia
figo za mjamzito hushindwa kabisa kufanya kazi, mjamzito kupata kiharusi
(stroke) au kupoteza maisha kabisa.
Kwenye kumzalisha mama mwenye kifafa cha mimba njia mbalimbali
huweza kutumika kutegemeana na hali ya mjamzito.
0 comments:
Post a Comment