Mfanyabiashara aliyejulikana kwa jina
moja la JAPHET amekamatwa na kikosi maalum kinachohusisha TRA , POLISI na
MAAFISA WA KILIMO akiwa anavusha mahidi kwa njia ya panya kutoka nchini Malawi
bila ya kufuata utaratibu wa sheria.
Tukio
hilo limetokea mnamo tarehe 29.01.2017 majira ya saa 4:30 asubuhi, katika mpaka
wa nchi ya Malawi na Tanzania wa Kasumulo Wilayani Kyela, kinyume
na sheria za uingizaji chakula nchini.
Mahidi hayo yamekamatwa yakiwa kwenye gari moja aina ya Canter
na mengine yalikuwa yamehifadhiwa kwenye 'store'.
Wakati wa uchukuaji wa mahidi 'store' kundi la wananchi
walijitokeza na walianza kuwazuia maafisa wa TRA kupakia mahindi hayo kwa kile
walichodai kuwa wanauziwa mahindi hayo kwa bei rahisi.
Kutokana na hali hiyo Polisi walilazimika kutumia mabomu ya
machozi ili kuwatawanya wananchi hao na baadaye hali kurejea kuwa shwari.
Jeshi la Polisi mkoani Mbeya limesema linaendelea na ufuatiliaji
wa karibu ili kubaini wafanyabiashara wenye tabia kama hiyo.
0 comments:
Post a Comment