Wizara ya mashauri ya nchi za kigeni nchini Sudan imemuita mwanabalozi wa
Marekani mjini Khartoum kupinga hatua ya Rais Donald Trump ya kuwapiga marufuku
raia wa nchi hiyo kuingia Marekani.
Sudan inasema kuwa
hatua hiyo ni ishara mbaya baada ya hatua nzuri za kuboresha uhusiano wa
mataifa hayo mawili ikiwemo kupunguza vikwazo vya kiuchumi na ushirikiano katika
vita dhidi ya Ugaidi.
Amri hiyo ya Trump
ilitikiza mpango mzima ya wakimbizi wa Marekani baada ya kutangazwa marufuku ya
siku 90 ya usafiri wa raia kutoka Somalia, Sudan, Libya, Syria, Iran, Iraq na
Yemen.
0 comments:
Post a Comment