Wednesday 25 January 2017

UMEME WAKATIKA GHAFLA TANZANIA…

Maeneo yote yaliyounganishwa kwenye mfumo wa taifa wa kusambaza umeme Tanzania, asubuhi yameathiriwa na kukatika kwa ghafla kwa umeme.

Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania limesema tatizo hilo limesababishwa na hitilafu katika mtambo wa kupooza na kusambaza umeme eneo la Ubungo, Dar es Salaam.
Umeme ulikatika mwendo wa saa kumi na mbili unusu asubuhi,ikielezwa ni kutokea kwa hitilafu katika katika mtambo wa kilovolti 220 ambao ni wa kupoozea na kusambaza umeme uliopo Ubungo.




0 comments:

Post a Comment