Imeelezwa kuwa uhaba wa
mahakimu katika Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi imefanya kila hakimu katika
mahakama hiyo kuwa na mzigo wa mashauri 400 kwa mwezi mmoja.
kufuatia hali hiyo,
mahakama imeomba Mabaraza za Ardhi ya Vijiji, Kata, na ya Nyumba ya Wilaya
kuondolewa katika ngazi ya utoaji hukumu na usuluhishi wa kesi za migogoro ya
ardhi nchini ili kusaidia kuharakisha utatuzi wa migogoro ya ardhi
Akizungumza na Hot Mix leo katika maonesho ya wiki ya sheria
yanayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam, Naibu
Msajili Mfawidhi wa Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi, Frank Mahimbali ambaye
amesema, kuwepo kwa vyombo vingi vya usuluhishi na maamuzi katika utatuzi wa
migogoro ya ardhi nchini kunachangia ucheleweshwaji wa kusikiliza mashauri ya
migogoro ya adhi.
Amesema, ni vyema shughuli za utatuzi wa migogoro ya ardhi
ikaachiwa Mahakama pekee kutokana na maamuzi mengine yanayofanywa na ngazi hizo
kuwana mgongano wa kimaslahi baina ya wizara na taasisi zinazosimamiwa na ngazi
hizo na kuchangia ucheleweshwaji wa kesi.
Aidha Naibu Msajili Mfawidhi wa Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi
Frank Mahimbali, ameeleza kuwa kwa sasa Mahakama Kuu ya Divisheni ya Ardhi ina
mahakimu wa 5 pekee huku idadi ya mashauri ikiwa ni 2,217 jambo
linalopelekea hakimu mmoja kusikiliza mashauri 400 kwa mwezi hivyo kuiomba
serikali kuongeza mahakimu katika mahakama hiyo.
0 comments:
Post a Comment