Rais mpya wa Gambia Adama Barrow amemteua
mwanamke mwenye ushawishi mkubwa, ambaye aliwahi kuwa mshirika wa aliyekuwa
rais wa taifa hilo Yahya Jammeh kabla ya kujiunga na upinzani ulioshinda
uchaguzi kuwa makamu wake wa urais.
Aidha mwanamke huyo
kwa jina Fatoumata Jallow-Tambajang alimtishia kiongozi huyo kwa kumfungulia
mashtaka.
Lakini watu wanatilia
shaka iwapo bi Tambajang mwenye umri wa miaka 68 anahitimu kupewa wadhfa huo
kutokana na umri wake.
Bi Tambajang aliwahi
kuhudumu kama waziri wa afya na maswala ya kijamii wakati wa utawala wa Yahya
Jammeh lakini akalazimika kwenda mafichoni baada ya kukosana naye.
Baadaye alikuwa kiungo
muhimu katika kuanzisha upinzani uliomshinda Jammeh mnamo tarehe mosi mwezi
Disemba, na alikuwa wa kwanza kumtishia kwamba atamfunguliwa mashtaka kwa
uhalifu aliotekeleza wakati wa utawala wake,wito unaoenda kinyume na rais Adama
Barrow.
0 comments:
Post a Comment