Thursday 19 January 2017

OBAMA AMALIZA MUDA WAKE IKULU YA WHITE HOUSE..

Rais Barack Obama wa Marekani amekuwa na mkutano wake wa mwisho na waandishi habari Ikulu mjini washington, tukio la mwisho la shughuli zake rasmi , kabla ya kumkabidhi madaraka Rais mteule Donald Trump.

Obama aligusia juu masuala ya kimataifa , akisema ana wasiwasi kuhusu suluhisho la dola mbili kati ya Israel na Palestina na kuzungumzia kuhusu hali ya baadaye, akisema atatumia muda wake zaidi kwa ajili ya mke wake na familia.
Pia aligusia kuhusu uhuru wa vyombo vya habari, akisema ni sehemu ya Marekani inavyofanyakazi.

Obama na familia yake ataondoka kwenda Palm Springs , Califonia , kesho Ijumaa baada ya kuapishwa kwa rais mteule Donald Trump kuwa rais wa 45 wa Marekani.

0 comments:

Post a Comment