Thursday 26 January 2017

MEXICO: HATUTALIPIA UKUTA WA DONALD TRUMP..!!

Nchi ya Mexico imesema kuwa haitalipia gharama ukuta uliopendekezwa kujengwa, na rais wa Marekani Donald Trump.

Kauli hiyo imetolewa na rais wa taifa hilo Enrique Pena Nieto kupitia Runinga nchini humo,huku akishutumu mpango huo wa Donald Trump.
Hata hivyo rais huyo hakuzungumzia iwapo atafutilia mbali ziara yake ya Marekani,ambapo anatarajiwa kukutana na rais Donald Trump tarehe 32 Januari.
Trump tayari amesaini agizo la urais la kujenga ukuta kati ya Marekani na Mexico, na amesisitiza kuwa Mexico itailipa Marekani kwa ukuta huo.

0 comments:

Post a Comment