This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Tuesday 30 June 2015

Sikiliza Antenna show ya Juma tatu Tar 29-6 na Kiwa le 11.

Kiwa Strong''Kiwale11"
Show inakwenda hewani kila juma tatu mpaka ijuma kuanzia saa  kumi kamili jioni mpaka saa kumi na mbili na nusu jioni.

Ina mchanganyiko wa habari,burudani,mahojiano na mazungumzo mbali mbali,unaweza kuisikiliza au kuishusha hapo chini kwa kubonyeza Play.

Facebook yafungua Ofisi Afrika kusini....!!!

Kwa mara ya kwanza Facebook imefungua ofisi yake barani Afrika, Johannesburg nchini Afrika kusini ikiwa ndio makao makuu.

Monday 29 June 2015

Mfungwa aliyetoroka New York akamatwa..

David Sweat aliyekamatwa baada ya kutoroka gerezani katika jimbo la New York alikokuwa akitumikia adhabu ya kifungo kutokana na makosa ya mauaji
Polisi nchini Marekani wamempiga risasi na kumkamata mfungwa aliyetoroka gerezani katika jimbo la New York alikokuwa amefungwa kutumikia adhabu kutokana na makosa ya mauaji wiki tatu zilizopita.

AU yajiweka kando uchaguzi wa Burundi……

Makao makuu ya Umoja wa Afrika, Addis Ababa,Ethiopia
Umoja wa Afrika umesema hautawapeleka waangalizi wake wa uchaguzi katika uchaguzi wa wabunge wa Burundi, unaofanyika leo kwa sababu masharti ya uchaguzi huru na wa haki hayajazingatiwa.

Friday 26 June 2015

Mtu mmoja amechinjwa Ufaransa………

Mtu mmoja amechinjwa Ufaransa
Mtu mmoja amechinjwa na mwengine akajeruhiwa vibaya,baada ya shambulizi la kiislamu katika mji wa Lyon Ufaransa.

Watoto waliwa na fisi, wafa…

Watoto wawili wenye umri wa kati ya miaka miwili na mitano wameuawa na fisi katika Kijiji cha Mnkola, Kata ya Ibihwa wilayani Bahi Mkoa wa Dodoma katika matukio mawili tofauti.

Alioa siku 3 tu kabla ya kuaga dunia……!!

Alioa siku 3 tu kabla ya kuaga dunia
Kijana mmoja barubaru alimuoa mpenzi wake siku tatu tu kabla yake kuaga dunia kutokana na Saratani ya damu lukaemia.

Kobe huenda wakaangamia Madagascar....!

Aina moja ya Kobe wanaowindwa na wawindaji haramu nchini Madagascar wako katika hatari kubwa ya kuangamia.
Sasa wanaharakati wa kulinda mazingira wameanza kuweka alama kwenye kauri za kobe hao waliosalia kwa nia ya kuharibu uzuri wao katika macho ya wawindaji haramu.

Kobe mmoja anauzwa katika soko la chini kwa chini kwa dola elfu 37 hivi.

Thursday 25 June 2015

Wapatikana hai siku 5 baada ya ajali ya ndege...

Bi Maria Nelly Murillo 18 na mwanawe wa kiume mwenye umri wa mwaka mmoja, walipatikana siku 5 baada ya ndege ya Cessna waliokuwa wakisafiria kuanguka katika msitu mkubwa ulioko katika jimbo la Choco.

Mtoto auwawa baada ya kubakwa Dar…………


Mtoto anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka mitano hadi sita, ameuwa kikatili jijini Dar es salaam baada ya kubakwa na kisha kunyongwa shingo huku akidaiwa kunyofolewa sehemu za siri.

Akamatwa uwanja wa ndege Dar na kobe 173…


Jeshi la Polisi Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere,linamshikilia raia wa Kuwait Hussein Mansoor, kwa kukutwa na kobe hai 173 aliokuwa akiwasafirisha kueleka nchini kwake.

Uyoga unazuia mtu kunenepa :Utafiti……

Uyoga unatumika nchini Uchina kama dawa ya kupunguza unene.

Wednesday 24 June 2015

Facebook kukutambua bila picha ya uso...!!!

Tayari mtandao huo wa kijamii wa Facebook unakusanya taarifa kutoka katika picha zako ili kubaini migao ya maoni kutoka kwa marafiki wako pale wanapoweka mtandaoni picha.

Kondomu inayotambua maambukizi ya Zinaa...!!

Wanafunzi katika shule moja nchini Uingereza, wameunda mipira ya kondomu inayowaonya watumiaji wanapojamiana na mtu aliyeambukizwa maradhi ya zinaa.


Usikose kusoma gazeti la TABIBU kesho alhamisi likiwa limesheheni habari kemkem kuhusu afya.

TABIBU michezo wiki hii.!!!

Hollande achunguzwa na NSA…..?

Mtandao wa Wikileaks umechapisha nyaraka zinazoonyesha kuwa chombo cha upelelezi cha Marekani NSA kimemchunguza rais wa Ufaransa, Francois Hollande, na marais wawili waliokuwa kabla yake.
Pata taarifa zaidi kwa kubonyza play hapa chini

Kupambana na utipwatipwa ni wajibu wa jamii:WHO..



Shirika la Afya Duniani WHO jana limezindua ripoti yake ya muda kuhusu kusitisha utipwatipwa wa watoto, ikisema idadi ya watoto wanaokumbwa na unene huo wa kupindukia imeongezeka kwa asilimia 47 tangu mwaka 1980, hasa kwenye nchi zenye kipato cha juu.

Wanaovalia suruali za kubana waonywa…

Suruali ndefu aina ya jinsi zinazobana, zinaweza kusababisha madhara makubwa kwa mishipa na misuli, madaktari wameonya.

Mwalimu mkuu ashiriki ngono na wanafunzi……!!

Mwalimu mmoja mkuu, amekiri kufanya ngono na wavulana wawili wenye umri mdogo.
Anne Lakey mwenye umri wa miaka 55 kutoka eneo la Stanley katika kaunti ya Durham, amekanusha makosa 13 dhidi yake ya kufanya matendo ya aibu kwa kushikashika sehemu za siri wavulana wawili miaka ya themanini.

Zaidi ya watu mil 1 wanatumia dawa za kulevya China..!

China ni nchi ambayo adhabu zake kwa wahusika wa dawa za kulevya hazina salia mtume kabisa yaani ukishikwa basi adhabu ya kifo inachukuwa hatamu.

Tuesday 23 June 2015

Mazungumzo ya amani Burundi kuanza tena…

Rais Pierre Nkurunziza
Mazungumzo ya kutafuta amani nchini Burundi, yanatarajiwa kuanza tena leo baada ya kusitishwa kwa siku kadhaa.
Mazungumzo hayo ni kati ya serikali, vyama vya upinzani na makundi ya kutetea haki za kibinaadamu, yenye lengo la kumaliza mgogoro wa kisiasa uliozuka kufuatia azma ya Rais Pierre Nkurunziza ya kuwania muhula wa tatu.

Mazungumzo hayo yanasimamiwa na msuluhishi mpya Abdoulaye Bathily kutoka Senegal.
Kutoka Bujumbura Burundi sikiliza taarifa ya Ramadhan Kibuga anasimulia.

Sherehe za nyama ya mbwa zaanza Uchina….!

Sherehe ya kula nyama ya mbwa kusini magharibi mwa China,imeanza huku kukiwa na pingamizi miongoni mwa wanaharakati wa haki za wanyama.
Takriban mbwa 10,000 watachinjwa na nyama yao kuliwa katika sherehe hizo,zitakazofanyika katika eneo la Yulin mkoa wa Guangxi siku ya jumapili na jumatatu.

Hii inafanyikia ili kuadhimisha kuanza kwa msimu wa joto kulingana na vyombo vya habari vya kitaifa.

Maji ya ATM yazinduliwa nchini Kenya……

Wakazi wa kitongoji duni cha Mathare katika mji mkuu wa Kenya Nairobi, sasa wanaweza kupata maji safi ya kunywa na kwa matumizi mengine.

Monday 22 June 2015

Waendesha boda boda hatarini kuwa wagumba…!!!

Madereva wa kiume wa pikipiki maarufu kama bodaboda na wengine wanaotumia usafiri huo kwa muda mrefu wapo katika hatari ya kuwa wagumba.

Kuhusu vurungu alizofanyiwa Rais Jacob Zuma bungeni..!!

Rais Jacob Zuma
Tarehe 19 June mwaka huu Bunge la South Africa liliingia kwenye headlines katika vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii baada ya baadhi ya viongozi kutoka chama cha upinzani kuanzisha vurugu zilizo pelekea kuairishwa kwa Bunge hilo siku ya ijumaa.

Bunge la Afghanistan lashambuliwa……

Bunge Afghanistan
Ripoti zinasema kuwa kumetokea mlipuko mkubwa karibu na bunge la Afghanistan huko KabulPicha za runinga zinaonyesha wabunge wakikimbilia usalama wao.

ANTENNA SHOW YA RADIO 5 IJUMAA TAR 19-6-2015..

Kiwa Strong"Kiwale 11"
Nimekuwekea hapa tena show ya Antenna inayokujia kila siku za juma tatu mpka ijuma kuanzia saa kumi jioni mpa kumi n ambili na nusu jioni,ni show kachumbari yenye mchanganyiko wa info kibao.
Bonyeza play hapa chini kuisikiliza show hiyo mdau wangu pande zote za tanzania.



HII HAPA NGOMA MPYA YA MCHINA BOY-JISOGEZE

Nimekuwekea hapa ngoma mpya ya kijana anafahamika kama Mchina boy akiwa amewashirikisha wakali War wil na Shebby Love,ngoma inakwenda kwa jina la JISOGEZE.

Unaweza kuisikiliza ngoma hiyo hapa chini pia kuishusha uendelee kusaport Good Music Uzidi kupenya kila kona.


Utafiti:Watoto waongo ni werevu...!!!

Wanasayansi nchini Uingereza wanasema kuwa wana ushahidi kwamba watoto wanaodanganya bila mtu kugundua wana kumbukumbu nzuri ikilinganishwa na wale wasiodanganya.

Friday 19 June 2015

Jimbo lingine Marekani lahalalisha matumizi ya bangi……!!!

Gavana wa Jimbo la Delaware nchini Marekani Jack Allan Markell, leo ameingia kwenye Headlines baada ya kusaini Sheria inayoruhusu matumizi ya bangi.

ANTENNA SHOW YA JANA TAR 18-6-2015 HII HAPA..!!

Kiwa Strong "kiwale 11"
Kama jana ulipitwa  na show ya Antenna ya Radio 5,basi nimekuwekea hapa kumbuka ni siku tano za wiki juma tatu mpaka ijumaa,kuanzia saa kumi kamili jioni mpaka kumi na mbili na nusu jioni.

Bonyeza Play hapa chini kusikiliza kilicho hapen jana kwenye show With Kiwa Strong.



Watu 25 wafa kwa kunywa gongo India..!!!

Mtu aliyekunywa pombe haram akihudumiwa
Watu wapatao 25 wamekufa katika mji wa Mumbai nchini India, baada ya kunywa pombe haramu aina ya Gongo na wengine wengi wamelazwa hospitali.

Chad yapiga marufuku vazi la hijabu…!!!!

Ikiwa jana waislamu katika maeneo mengi dunia wameanza mwezi mtufu wa  ramadhani,nchini chad imetolewa amri ya mtu yoyote kutovaa vazi la hijabu.

Thursday 18 June 2015

Roboti kuchukua kazi za raia Australia…!!!

Roboti la muuguzi
Takriban asilimia 40 ya kazi nchini Australia ambazo zipo kwa sasa huenda zikapotea katika kipindi cha kati ya miaka 10 hadi 15 ijayo .

Ramadhani imeanza leo maeneo mengi ya dunia!!

Waislamu katika nchi nyingi duniani leo wamenza funga ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Sura ya mwanamke kuwa katika noti mpya……

Benki Kuu ya Marekani

Kwa mara ya kwanza katika kipindi cha zaidi ya karne moja, noti mpya ya dola kumi nchini Marekani itakuwa na picha na mwanamke.

Shambulio lafanyika Kanisa la Marekani…!!

Shambulio katika Kanisa la Kihistoria la Methodist katika jimbo la South Carolina, Marekani
Polisi katika jimbo la South Carolina nchini Marekani, wanamsaka mtu mwenye silaha alihusika katika shambulio katika Kanisa la Methodist lililo katika eneo la Charleston.

Wednesday 17 June 2015


Je unakifahamu kiungo cha Giligilani? Usikose nakala yako ya gazeti la TABIBU kesho alhamisi likiwa limesheni habari kemkem kuhusu afya.
                                                          TABIBU michezo wiki hii.!!!

Serikali ya muungano ya Palestina kujiuzulu...!!!

Rais wa mamlaka ya ndani ya Palestina Mahammud Abbas ametangaza kuwa serikali ya muungano aliyounda na Hamas mwaka jana itajiuzulu.
Abbas hakutangaza ni lini hasa hatua hiyo itachukuliwa lakini inatarajiwa hatua hiyo itatekelezwa katika kipindi cha saa ishirini na nne zijazo.
Abbas amesema uamuzi huo wa kuivunja serikali hiyo ya muungano ni kwa sababu Hamas haijairuhusu serikali kufanya kazi katika ukanda wa Gaza.
Serikali ya muungano kati ya tawi la kisiasa la Hamas na chama cha Fatah cha Abbas iliundwa mwezi Aprili mwaka jana kabla ya vita kati ya wanamgambo wa Hamas na Israel katika ukanda wa Gaza.
Hata hivyo serikali hiyo imekuwa haifanyi kazi vyema kutokana na malumbano ya jinsi ya kuujenga tena ukanda wa Gaza ulioharibiwa wakati wa vita vya mwaka jana na kuhusu masuala mengine.

Wanafunzi Somalia wafanya mtihani wa taifa baada ya miaka 25..!!!

Mtihani wa kwanza Somalia katika miaka 25
Zaidi ya wanafunzi elfu 70 walifanya mitihani ya kidato cha nne katika maeneo ya kusini na kati
mwa Somalia, ikiwa ni mitihani ya kwanza ya kitaifa katika kipindi cha miaka 25.

China yaipa Takukuru vifaa vya bilioni 3….

Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk. Edward Hoseah.
Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China, imeikabidhi Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) vifaa vya kiufundi vya Sh. bilioni tatu, kwa ajili ya kuiongezea ufanisi zaidi taasisi hiyo katika vita dhidi ya vitendo vya rushwa.

Raia Nigeria wapinga posho za wabunge…!!!


Wananchi wa Nigeria wamechukizwa na taarifa kwamba wabunge wamejiidhinishia mamilioni ya dola kwa ajili ya posho ikiwemo ya mavazi.

Tuesday 16 June 2015

Kiongozi wa Al Qaeda nchini Yemen auawa…!!

Kiongozi wa Al Qaeda nchini Yemen auawa
Tawi la kundi la Al Qaeda nchini Yemen limethibitisha kuuawa kwa kiongozi wake wakati wa shambulizi la ndege isiyokuwa na rubani ya Marekani.

Askofu kushtakiwa kwa kudhulumu watoto…!!!

Askofu Josef Weslowski kushtakiwa kwa kudhulumu watoto

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis, ameonekana kuanza kuwakabili makasisi waliotuhumiwa kwa sakata ya ngono.

Unafahamu kwa nini kuna siku ya mtoto wa Africa…!!!



Tarehe 16 Juni ya kila mwaka Tanzania huungana na Nchi nyingine za Afrika kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika.

Monday 15 June 2015

Kasisi basha aishtaki kanisa kumbagua…!!!

Kasisi basha aishtaki kanisa kumbagua

Kasisi mmoja ambaye alinyimwa leseni ya kufanya kazi kama mhudumu katika zahanati ya afya kwa misingi ya kuwa katika ndoa ya jinsia moja,amelishtaki kanisa kwa kumbagua.

Sikiliza Antenna show ya radio 5 hapa.!!

Hii show inakwenda hewani kila siku za juma tatu mpaka ijuumaa saa kumi jioni mpaka kumi na mbili na nusu jioni.Bonyeza play hapa chini kuisikiliza show iliyoruka Tar 10-6-2015.

Wapenzi wakongwe zaidi duniani waoana…!!!

Mwanaume mmoja Muingereza mwenye umri wa miaka 103 ameingia katika daftari za historia kwa kuwa bwana harusi mkongwe zaidi duniani.

Friday 12 June 2015

Mkurugenzi mkuu wa Twitter kujiuzulu...!!!

Mkurugenzi mkuu wa Twitter, Dick Costolo, ana nia ya kujiuzulu ifikapo mwisho wa mwezi huu wa Juni, kufuatia shinikizo kutoka kwa wawekezaji, ambao wanalalamikia ukuaji polepole wa mtandao huo wa kijamii.

Siku ya Albino kuazimishwa duniani kwa mara ya kwanza June 13-2015....

Ikiwa kesho ni maadhimisho ya kwanza kabisa ya siku ya kuhamasisha jamii kuhusu haki ya watu wenye ulemavu wa ngozi Albino, kamishna Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Zeid Ra'ad Al Hussein,amesema ni fursa ya kutambua vipaji adhimu walivyo navyo kundi hilo.