Kwa
mara ya kwanza Facebook imefungua ofisi yake barani Afrika, Johannesburg nchini
Afrika kusini ikiwa ndio makao makuu.
Mwanadada Nunu Ntshingila ndie
atakae ongoza ofisi hiyo itakayo jikita katika kutafuta njia mbali mbali za
kuongeza ushirikiano na wafanya biashara wa barani humo.
Tayari watumiaji wa facebook
barani Afrika ni milioni 120, ofisi hiyo mpya inalenga kuongeza idadi ya
watumiaji wake nchini Kenya, Nigeria na Afrika Kusini.
Nunu Ntshingila ndiye mkurugenzi
mkuu wa ofisi hiyo,ambae amesema kuwa mkakati wa kupanua uwekezaji wao hasa
katika matangazo ni mipango mikubwa ya kutanua biashara pamoja na bara la Ulaya
na maeneo ya Mashariki ya Kati.
Barani Afrika kuna mtumiaji mmoja
kati ya watano wa intanenti na inatarajiwa idadi hiyo kukua mara mbili zaidi
kwa watumiaji wa simu za mkononi ifikapo mwaka 2020.
Asilimia 80% ya wanao tumia
facebook ni wale wenye kupata huduma hiyo kupitia simu zao za mikoni.
Facebook anasema pia ina mipango
madhubuti ya kuongeza wateja kutoka nchi za Senegal, Ivory Coast, Ghana,
Tanzania, Rwanda, Uganda, Zambia, Msumbiji na Ethiopia ili kufikia malengo
yake.
0 comments:
Post a Comment