Ikiwa kesho ni maadhimisho ya kwanza kabisa ya siku ya kuhamasisha
jamii kuhusu haki ya watu wenye ulemavu wa ngozi Albino, kamishna Mkuu wa haki
za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Zeid Ra'ad Al Hussein,amesema ni fursa ya
kutambua vipaji adhimu walivyo navyo kundi hilo.
Siku hiyo inaadhimishwa tarehe 13 mwezi huu kwa kutambua umuhimu wa kulinda haki za watu wenye ulemavu wa ngozi, wakati huu ambapo wanakumbwa na madhila ikiwemo kuuawa kwa imani za kishirikina.
Kamishna Zeid amesema ni lazima kutambua kuwa watoto wanaozaliwa na ulemavu wa ngozi, ni kutokana na jenetiki zilizopo kwenye familia zao,lakini ukosefu wa uelewa huwatumbukiza kwenye madhila kutokana na rangi ya ngozi yao.
Nchini Tanzania siku hii itaazimishwa mkoani Arusha,na inazaniwa kuwa huenda Arusha imepewa heshima hiyo kutokana na kutokuwa na matukio ya kuuwawa kwa Albino,ikilinganisha na mikoa mingine ya Tanzania.
Kiwale11.blogspot.com imepiga story na Vick Mtetema mkurugenzi
wa shirika la Under the same Sune, ambalo linapambana na vitendo vya
ukatili kwa watu wenye ulemavu wa ngozi,msikie hapa chini kwa kubonyeza play anazungumzia
kuhusiana na siku hiyo ya watu wenye ulemavu wa ngozi duniani.
0 comments:
Post a Comment