Uyoga
unatumika nchini Uchina kama dawa ya kupunguza unene.
Kwa miaka na
mikaka uyoga umekuwa ukitumika nchini humo kama dawa ya kupunguza unene katika
wanyama, hayo yamesemwa na watafiti nchini Taiwan.
Utafiti huo uliochapishwa
katika jarida la mawasiliano ya mazingira, unabaini kuwa madini ya Ganoderma
Lucidum iliyoko ndani ya uyoga, hupunguza taratibu uwezo wa mtu kupata uzani
mkubwa kwa kutatiza bakteria ndani ya utumbo.
Watafiti
wanapendekeza kuwa uyoga hatimaye utatumika katika matibabu ya kupunguza uzito.
Wataalam wanasema
kuwa sayansi hiyo ni nzuri,lakini kuweka maji yanayotokana na uyoga kwenye
mikebe ya cola hakutawasaidia watu kupunguza uzani.
G. lucidum
imekuwa ikiuzwa tangu jadi kama kichocheo cha "kiafya na kurefusha
maisha" hayo ni kwa mjibu wa watafiti katika chuo kikuu cha Chang Gung.
0 comments:
Post a Comment