Thursday 18 June 2015

Shambulio lafanyika Kanisa la Marekani…!!

Shambulio katika Kanisa la Kihistoria la Methodist katika jimbo la South Carolina, Marekani
Polisi katika jimbo la South Carolina nchini Marekani, wanamsaka mtu mwenye silaha alihusika katika shambulio katika Kanisa la Methodist lililo katika eneo la Charleston.
Habari ambazo bado hazijathibitishwa kutoka vyombo vya habari vya eneo hilo, zinasema kumekuwepo na vifo kadha.
Polisi huko Charleston wanasema mtuhumiwa ni mzungu mmoja akiwa katika umri wa miaka ya ishirini.

Shambulio hilo limefanyika katika Kanisa la Emanuel African Methodist Episcopal Church, moja ya makanisa kongwe ya Waafrika Wamarekani nchini Marekani.

0 comments:

Post a Comment