Shirika la
Afya Duniani WHO jana limezindua ripoti yake ya muda kuhusu kusitisha
utipwatipwa wa watoto, ikisema idadi ya watoto wanaokumbwa na unene huo wa
kupindukia imeongezeka kwa asilimia 47 tangu mwaka 1980, hasa kwenye nchi zenye
kipato cha juu.
Kwa mujibu wa WHO mwelekeo huo unaanza kuongezeka pia
kwenye nchi zinazoendelea.
Ripoti hiyo
iliyoandaliwa na kamisheni maalum kuhusu suala hilo,inaeleza kwamba utipwatipwa
si kosa la watoto,bali hutokana na mazingira wanamoishi ambayo yanawashawishi
kula vyakula venye sukari na mafuta zaidi bila kusahau vyakula walivyopatiwa
wakiwa wadogo au hata kabla ya kuzaliwa.
Ripoti hiyo
inasema ni wajibu wa jamii kupunguza hatari za utipwatipwa kwa watoto, afya ya
mtoto ikiwa ni moja ya haki zake za msingi.
Miongoni mwa mapendekezo ya ripoti hiyo ni kuelimisha
watoto shuleni,kuhusu lishe nzuri kwa afya, kusaidia shule kwenye maeneo yenye
kipato cha chini kuwapatia watoto milo mizuri kwa afya au kuweka kiwango cha
juu cha ushuru juu ya vinyaji venye sukari.
0 comments:
Post a Comment