Friday 19 June 2015

Jimbo lingine Marekani lahalalisha matumizi ya bangi……!!!

Gavana wa Jimbo la Delaware nchini Marekani Jack Allan Markell, leo ameingia kwenye Headlines baada ya kusaini Sheria inayoruhusu matumizi ya bangi.

Kwenye Sheria hiyo inakataza tu kuvuta sehemu ya watu wengi na kama ukikamatwa umekiuka kanuni hiyo,faini yake imepunguzwa pia kutoka Dola elfu 1 na 150 mpaka Dola mia 1 tu.
Jumla ya Majimbo ambayo mpaka sasa wamehalalisha kabisa matumizi ya Bangi ndani ya Marekani yako kama 23 hivi.
Moja wapo ni Jimbo la Colorado ambalo walifanikiwa  kukusanya kodi ambayo ni Dola Mil.15 (zaidi ya Bil 27 Tshs) kutokana na mauzo ya bangi ndani ya kipindi cha mwaka mmoja.

Hapa kwetu ishu hiyo iliingia Bungeni Dodoma May 26 2015,wakati Mbunge Cristowaja Mtinda aliuliza swali kuhusu Bangi kuhalalishwa kwa vile wapo wanaoitumia kama dawa na wengine chakula.
Jibu likatolewa na Naibu Waziri Juma Nkamia,kwamba Serikali haiko tayari kufanya Bangi iwe halali ndani ya TZ bonyeza play hapa chini usikilize bangi ni nini?


0 comments:

Post a Comment