Rais wa mamlaka ya ndani ya Palestina Mahammud Abbas ametangaza kuwa serikali ya muungano aliyounda na Hamas mwaka jana itajiuzulu.
Abbas hakutangaza ni lini hasa hatua hiyo itachukuliwa lakini inatarajiwa hatua hiyo itatekelezwa katika kipindi cha saa ishirini na nne zijazo.
Abbas amesema uamuzi huo wa kuivunja serikali hiyo ya muungano ni kwa sababu Hamas haijairuhusu serikali kufanya kazi katika ukanda wa Gaza.
Serikali ya muungano kati ya tawi la kisiasa la Hamas na chama cha Fatah cha Abbas iliundwa mwezi Aprili mwaka jana kabla ya vita kati ya wanamgambo wa Hamas na Israel katika ukanda wa Gaza.
Hata hivyo serikali hiyo imekuwa haifanyi kazi vyema kutokana na malumbano ya jinsi ya kuujenga tena ukanda wa Gaza ulioharibiwa wakati wa vita vya mwaka jana na kuhusu masuala mengine.
0 comments:
Post a Comment