Suruali ndefu aina ya jinsi zinazobana, zinaweza kusababisha madhara makubwa kwa mishipa na misuli, madaktari wameonya.
Hayo ni kwa mjibu wa jarida la
Neurology, ambalo huandika habari kuhusu upasuaji.
Alichuchumaa kwa muda mrefu sana
ili kuondoa bidhaa ndani ya kabati,alipokuwa akijiandaa kuhama nchini
Australia.
Ilipofika jioni miguu yake
ilikuwa imekufa ganzi,na akashindwa kutembea.
Madaktari waanamini kuwa mwanamke
huyo alipatwa na maradhi yanayojulikana kama compartment syndrome, ambayo
yalisababishwa na suruali yake ndefu yenye kubana mno.
Ugonjwa huo ni mbaya sana na
husababishwa na kuvuja kwa damu na kuvimba kwa misuli.
Tatizo hilo lilimfanya mwanamke
huyo kuteguka na kuanguka na akashindwa kuinuka,na kusalia ardhini kwa saa
kadhaa.
Alipofikishwa katika Hospitali ya Royal Adelaide, sehemu
ya chini ya miguu yake ilikuwa na uvimbe m'baya.
Ingawa miguu yake ilikuwa na joto
na damu ilikuwa ikisambazwa vyema, misuli yake ilikuwa haina nguvu na ilikuwa
imeshapoteza hisia.
0 comments:
Post a Comment