Tuesday 11 August 2015

Joto kali layeyusha gari Italy…………..

Siku za hivi karibuni baadhi ya maeneo Stori za joto kuongezeka,zimekuwa zikichukua nafasi kubwa sana, nikukumbushe tu kwamba ilianza kule Dubai ambapo  joto lilipanda mpaka kufikia nyuzi 38, tukasikia Uingereza nako nyuzi joto nako zilipanda hadi kufikia 40 lakini kule india na kwenyewe joto lilipamda hadi kufikia nyuzi 45.

Sasa stori toka nchini Italy ni kwamba nyuzi joto limeongezeka kufikia nyuzi 37C, na hii imepelekea matukio na athari za jua yamekuwa yakiripotiwa sana nchini umo.

Moja ya stori toka huko ni hii ya sehemu za urembo wa gari dogo lililokuwa limeegeshwa, kuyeyuka kutokana na joto kali la jua.
Tukio lilinaswa kwenye picha na video na mtalii mmoja aliyekuwa anatoka hotelini kuelekea beach, na kisha kushangazwa kuona uji uji mzito unidondoka kutoka kwenye gari hilo, alipolikaribia gari hilo aligundua kuwa gari lilikuwa linayeyuka kutokana na joto kali la jua


Kitu hiki kimewashangaza watu wengi huku vyombo vingi vya usalama nchini humo, vimewaomba watu kupunguza kutoka nje na kwenda baharini na kufunga viyoyozi vitakavyowasaidia kupunguza joto.

0 comments:

Post a Comment