Shirika la
Dawa na Chakula nchini Marekani (FDA) limeidhinisha matumizi ya dawa ya kwanza
kabisa iliyoundwa mahususi kuwatibu wanawake ambao hawana hamu ya kufanya
mapenzi maarufu ''viagra ya wanawake''
Dawa hiyo inaviungo maalum vinavyofanya kazi kwa kuongeza
kemikali fulani akilini mwa wanawake ilikuimarisha hamu ya kutaka kufanya
mapenzi.
Flibanserin
inayotengezwa na kampuni ya kutengeneza madawa ya Sprout Pharmaceuticals
imeidhinishwa na FDA.
Sampuli moja ya dawa hiyo itakuwa ikiuzwa kwa jina
"Addyi" katika maduka ya madawa japo iliwasilishwa kwa shirika hilo
la FDA na kukataliwa.
Dawa hiyo ilikataliwa mara mbili kwa sababu ilikuwa
inasababisha watu walioimeza kusinzia mbali na visa kadha vya kuzirai.
Wanawake
waliojaribu dawa hiyo wameripoti ''kufikia kilele'' takriban mara moja kwa
mwezi.
Awali dawa hiyo ilikuwa ikitengenezwa na kampuni ya kuunda
madawa ya Ujerumani, Boehringer Ingelheim.
Lakini Sprout iliinunua baada ya kushindwa kuidhinishwa
nchini Marekani mara mbili.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa shirika hilo la FDA, dawa
hiyo imeundwa mahsusi kutibu ukosefu wa hamu ya kufanya mapenzi kwa wanawake hypoactive
sexual desire disorder (HSDD)'.
Dawa hiyo
hata hivyo itatolewa kwa mhitaji baada ya kupata ushauri wa daktari.
Madaktari wanatarajiwa kutoa dawa hiyo kwa wagonjwa wa
''female sexual interest ama arousal disorder (FSIAD).
Lakini dawa hiyo itaambatana na onyo kali la kiafya, kuhusu
uwezekano wa mwanamke kupata madhara ikiwa ataimeza pamoja na pombe.
Mojawapo wa mashirika ya kutetea haki za wateja limeunga
mkono hatua hiyo,lakini Shirika lingine limesema dawa hiyo ni hatari kwa
wanawake.
0 comments:
Post a Comment