Raia
wa Japan leo wanaadhimisha kumbukumbu ya miaka 70 tangu shambulio la kwanza la
bomu la Atomiki kutekelezwa mjini Hiroshima.
Takriban watu laki moja na
arobaini walikadiriwa kupoteza maisha baada ya Ndege ya Marekani kudondosha
bomu ambalo liliuharibu mji huo tarehe 6 mwezi Agosti mwaka 1945.
Watu elfu sabini walipoteza
maisha papo hapo, huku wengine wa idadi kama hiyo walipoteza maisha kutokana na
athari za mionzi ya sumu.
Katika hotuba yake, Waziri Mkuu
wa Japan Shinzo Abe alisema kumbukumbu ya Heroshima inasisitiza uhitaji wa
kufanya jitihada ya kupiga vita matumizi ya Nuklia.
Shambulio la Hiroshima
lilifuatiwa na shambulio jingine la bomu la Atomiki katika mji wa Nagasaki.
Japan ilijisalimisha siku kadhaa
baadae, hatua iliyomaliza vita ya pili ya dunia.
0 comments:
Post a Comment