Thursday 20 August 2015

Juma Kaseja ajiunga na Mbeya City……

Baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu bila timu, golikipa mkongwe na mahiri Juma Kaseja August 19 amesaini mkataba wa miezi sita wa kuitumikia klabu yaMbeya City kutoka Jijini Mbeya.


Mkataba wa Juma Kaseja wa kujiunga na klabu ya Mbeya City umesainiwa mbele ya meneja wake mpya Athumani Tippo.


Kabla ya kusaini mkataba na Mbeya City, Juma Kaseja alikuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha zaidi ya miezi nane, baada ya kuingia katika mgogoro wa kimkataba na iliyokuwa klabu yake ya zamani ya Yanga nakufanya kesi hiyo kutinga mahakamani.

0 comments:

Post a Comment