This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Tuesday, 31 March 2015

Abiria aliandika barua kwa Rubani..!!!!!

Ishu ya ajali ya ndege ya Germanwings ambayo ilipata ajali katika milima ya Alps Ufaransa imekuwa ikizungumziwa sana hasa kutokana na ishu hiyo kuonekana kwamba rubani mmoja aliebaki ndani ya chumba cha marubani kuiangusha ndege hiyo kwa makusudi.

Haya ni Maamuzi Mapya Australia baada ya kugundulika Rubani aliangusha Ndege kwa makusudi..!!!

Waziri mkuu msaidizi wa Australia Warren Truss ndio ametoa taarifa hii,baada ya ajali ya ndege ya Ujerumani kuangushwa kwa makusudi na Rubani msaidizi huko Ufaransa na kuua watu wote ndani

Njia za kuongeza kasi ya kompyuta


Kompyuta nyingi zinaponunuliwa huwa na kasi kubwa, lakini baada ya muda kasi hiyo huanza kupungua.Kuna njia mbalimbali za kuongeza kasi ya kompyuta yako na vifaa vingine kama simu za mikono na Ipad.

Hii ndiyo mitandao hatari kwa ‘madenti’

Tangu kuingia kwa miatandao ya kijamii nchini vijana wengi wamepata nafasi ya kuituma au kupokea ujumbe mfupi, picha na video kwa njia rahisi zaidi kuliko ilivyokuwa miaka 20 iliyopita.

Walimu witishia kugoma mkoani Kagera!!!

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
Chama cha walimu wilaya ya MISENYI mkoani Kagera wanatarajia kuitisha mgomo usiokuwa na kikomo kwa kutofundisha katika shule za msingi na

Polisi inamsikilia aliyemkata na jembe shingoni mtoto wa kaka yake.!!

Mwanamke mmoja Shida Ngai mwenye umri wa miaka 35 mkazi wa makambi katika manispaa ya Songea mkoani ruvuma, anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani humo kwa tuhuma za kumpiga na kisha kumkata kwa jembe kwenye

Friday, 27 March 2015

TAFITI:Kilimanjaro vinara wa kunywa viroba..!!!!Utafiti mpya umebaini kuwa wakazi wa Mkoa wa Kilimanjaro wanaongoza kwa unywaji wa pombe  hasa ya  viroba,

Mtoto wa miaka 2 aweka rekodi India..!!!

Amini usiamini mtoto mwenye umri wa miaka miwili ameweka rekodi ya taifa ya ulengaji shabaha kwa mishale nchini India.

Utafiti: Hali ya uchumi ya mtu mmojammoja nchini ni mbaya kuliko ilivyokuwa miaka 10 iliyopita..!!!

Hivi karibuni, Taasisi ya Repoa ilitoa utafiti wake unaoonyesha kuwa hali ya kiuchumi ya wananchi inazidi kuwa mbaya ikilinganishwa na ilivyokuwa miaka 10 iliyopita.

Thursday, 26 March 2015

Lowassa asema hawezi zuia Mafuriko kwa mikono!!!

Siku moja baada ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kumuonya aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa,kwa tuhuma za kukiuka Katiba na kuanza kampeni za Urais kabla ya muda, kiongozi huyo ameibuka na kudai kuwa hana njia ya kuwazuia watu wasimuombe agombee Urais.

Ndege za Marekani yashambulia Tikrit nchini Iraq......

Ndege za kijeshi za Marekani zimeanza kutekeleza mashambulizi makali, katika maeneo yenyeUsikose kusoma gazeti lako pedwa la TABIBU kuhusu habari za afya liko mtaani kwa bei ya sh. 500/=

Wednesday, 25 March 2015

Msimu mwingine wa Kilimanjaro Tanzania Music Awards.. 2015 Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kwa kushirikiana na Kilimanjaro Premium Lager wamezindua rasmi msimu mwingine wa tuzo za muziki Tanzania unaojulikana kama Kilimanjaro Tanzania Music Awards (KTMA).

Tanzania na Kenya zimetiliana saini kulinda na kutunza misitu

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mazingira na Maliasili nchini Kenya Richard Lusiambe (wakwanza kulia) akiongozana na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki nchini Tanzania Gladness Mkamba mara baada ya kutia saini makubaliano ya Tanzania na Kenya kupiga vita biashara haramu ya mbao pamoja na mazao ya misitu inayofanyika kupitia mipaka ya nchi hizo katika mkutano uliofanyika jijini Arusha.

Awaua wanawe na kuwaweka ndani ya Jokofu 
Mwanamke mmoja amekamatwa na polisi kufuatia mauaji ya wanawe wawili waliopatikana wamefungikiwa ndani ya jokofu.

Monday, 23 March 2015

Majanga Dar…Mvua yasababisha vifoo!!!!

Watu watano wamefariki dunia kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam, watatu kati yao wakiwamo wanafunzi wawili, wakipoteza maisha baada ya kibanda walichojihifadhi kujikinga na mvua kuangukiwa na nguzo ya umeme na kuwaunguza.

Lema asema Kinana amepigwa changa la macho Arusha.!!!
Siku moja baada ya Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana kuwapokea viongozi wawili akisema wanatoka Chadema na kumtuhumu Mbunge wa Arusha, Godbless Lema kuwa anatumia madaraka yake kujinufaisha na mali za umma, mbunge huyo amejibu akisema: “Kinana amepigwa changa la macho.”

Hizi hapa sababu 5 za Zitto Kujiunga ACT.!!!

Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe,ametaja sababu tano za kujiunga na chama cha ACT-Tanzania,huku akijigamba kuwa yeye ni mchapakazi na kwamba sasa mambo yote ni mbele kwa mbele.

Saturday, 21 March 2015

Jana Sauti ya furaha ilisikika duniani kote..!!!

Tarehe 20 Machi kila mwaka ni siku ya furaha duniani, Umoja wa Mataifa umeandaa kampeni ya kukusanya maoni ya watu kutoka duniani kote ikitaka wakijibu swali , Je sauti ya furaha ni ipi?

Mwana wa Whitney aondoshwa hospitalini..

Mwana wa aliyekuwa mwanamuziki wa 'rhythm n blues' marehemu Whitney Houston Bobbi Kristina Brown ameondoshwa katika hospitali ya chuo kikuu cha Emory na sasa yuko katika nyumba ya kurekebishia tabia katika jimbo la Atlanta,lakini uhaimisho huo sio ishara kwamba hali yake inaimarika.

Shilingi ya Tanzania yashuka thamani

Thamani ya shilingi ya Tanzania imeelezwa kuanguka kwa kiasi cha asilimia 7.9, hali ambayo imeelezwa kuchangiwa na sababu za kiuchumi za ndani na nje ya nchi.

Dr Joseph massawe mkurugenzi wa utafiti wa uchumi na sera katika bank ya tanzania kuhusiana na sababu za kuporomoka kwa thamani ya shilingi,msike hapa chini.

YAHOO kufunga Ofisi zake China..!!


Kampuni ya mtandao YAHOO inatarajiwa kufunga ofisi yake ya mwisho katika eneo la China bara.

Issue nzima ya Zitto kujiuzulu Ubunge.

 
Jana Kikao cha Bunge kilikuwa kikiendelea Dodoma, Mbunge Zitto Kabwe alikuwa mmoja ya Wabunge waliochangia katika mjadala uliokuwa unaendelea jioni ya jana kabla ya kupewa nafasi ya kusimama na kutoa maelezo binafsi.

Kenya Airways yapunguza safari zake TZ.!!

Airways Shirika la ndege la Kenya, Kenya Airways jana limeanza rasmi kupunguza safiri zake katika uwanja wa ndege wa Dar es Salaam kufuatia agizo la mamlaka ya anga ya Tanzania kuamuru shirika hilo kupunguza safari zake kutoka 42 kwa wiki hadi 14.

Friday, 20 March 2015

WhatsApp yasababisha mke kupewa talaka!!!

Mwanamume mmoja nchini Saudia amempa talaka mkewe kutokana na ujumbe wake katika mtandao wa WhatsApp.

Ugumu wa maisha ndio kipimo cha akili..!!!!!

Ugumu wa maisha unaongeza ubunifu,lakini wakati mwingine ubunifu mwingine unaweza kukuweka pabaya.

Usikose nakala yako ya gazeti la TABIBU wiki hii lipo mtaani kwa bei ya sh. 500/=Tanesco yatoa kauli kuhusu umeme kukatika mara kwa mara.........

Shirika la umeme nchni-Tanesco-limesema hakuna mgao wa umeme na kilichojitokeza kufuatia kukatika kwa umeme mara kwa mara kuanzia machi 15 ni uchakavu wa miundombinu ya umeme ikiwemo kuanguka kwa nguzo za umeme hususani katika maeneo ya makazi ya watu yasiyopimwa.

Mauwaji ya Albino ni Janga la Taifa Serikali yatangaza...

Serikali imewataka maafisa wa jeshi la polisi hapa nchini kutumia mbinu zote za kijeshi na miongozo katika kuhakikisha wanakomomesha mauji ya watu wenye ulemavu wa ngozi ambayo yamekuwa janga kwa taifa.

Thursday, 19 March 2015

Mwinjilist akutwa amewahifadhi wahamiaji haramu huko kilimanjaro.....
JESHI la Polisi mkoani Kilimanjaro linamshikilia Mwinjilisti wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),

Wednesday, 18 March 2015

Jimbo la Colorado lakusanya kodi ya Bangi zaid ya bil 24..l..Kwa Tanzania Sheria zimebanwa zaidi kuzuia matumizi ya dawa za kulevya,lakini kwa Marekani wao kuna Majimbo ambayo yaliruhusu matumizi ya Bangi, uhalali huu umeingiza Bangi kuwa bidhaa halali kabisa kutumiwa na kuuzwa kama ilivyo bidhaa nyingine Majimbo kama ya Washington DC,Alaska na jimbo la colorado.

Majaji 3 nje kwa kutizama video za ngonoMajaji watatu wamefutwa kazi kwa kutumia muda wao afisini kutizama filamu za ngono.

Tuesday, 17 March 2015

Harufu ya Choo yalazimu ndege Kutuaa dakika chache baada ya kuruka..!!

Ndege moja ya shirika la ndege la British Airways,ilikuwa ikielekea Heathrow Uingereza kutoka Dubai,imelazimika kutua kufuatia harufu mbaya iliyokuwa ikitokea kwenye choo.

TAKUKURU Kuwaanika mtandaoni wala Rushwa..
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imetangaza katika tovuti yake majina 287 ya washtakiwa waliopatikana na hatia katika kesi za rushwa.

Mwanamfalme wa Uingereza Prince Harry kuondoka jeshini Juni..

Mwanamfalme wa Uingereza Prince Harry amesema anaangalia mustakhabali mwingine wa maisha baada ya kuthibitika kuwa ataacha jeshi mwezi Juni.
Taarifa kutoka makazi ya kifalme ya Kensington imesema Prince Harry atamaliza utumishi wake wa miaka kumi jeshini baada ya wiki nne kwenda kutumikia katika jeshi la ulinzi la Australia, kuanzia mwezi April.
Mrithi wa nne katika mfuatano wa warithi wa kiti cha ufalme wa Uingereza amesema uzoefu wake jeshini utabakia katika maisha yake yote.

Prince Harry amesema bado alikuwa akitafakari ajira yake.
Prince Harry ameshiriki mapigano mara mbili nchini Afghanistan, vita vya karibuni kabisa ni pale aliposhiriki mwaka 2012 akiwa rubani wa helikopta ya kijeshi aina ya Apache.
Prince Harry ametajwa kuwa rubani aliyetoa msaada mkubwa kwa wapiganaji wa ardhini kwa kuwajali.

Unajua kwa nini unapiga mihayo...Kwa kawaida upigaji wa miayo huashiria kuchoka kwa mwili, akili au kujisikia kuchoshwa na jambo au hali fulani. Hali hii hutokea bila kutarajia wala haiepukiki, kama ilivyo kuhema. 

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa kuhusu miayo, binadamu huanza kupiga miayo tangu akiwa tumboni na umri wa wiki 11!

Kuna maelezo mengi tofauti kuhusu suala la kupiga miayo, lakini yanayovutia zaidi ni yale yanayofanywa na mtafiti wa Chuo Kikuu cha Princeton Marekani ambaye amegundua 

kuwa kitendo cha kupiga miayo huwa kinafanya kazi muhimu sana ya kuupoza ubongo.

Utafiti huo unasheheresha kwa kusema kuwa miayo huwa sawa na ‘reguleta’ ya kurekebisha joto la ubongo, pale joto linapokuwa limezidi kwenye ubongo kutokana na sababu mbalimbali, miayo hutokea kuupoza.

Imeelezwa kuwa watu wengi hupiga miayo wakati wa kipindi cha baridi kuliko kipindi cha joto kwa sababu kipindi cha baridi ubongo huchemka na kitendo cha kupiga miayo huwa kinatokana na mahitaji ya mwili ya kiasili ya kurekebisha hali ya joto kwenye ubongo.

Vile vile utafiti umeonesha kuwa binadamu anapokosa usingizi usiku, joto la ubongo huongezeka kutokana na kufikiri, hivyo anapoamka asubuhi hujikuta analazimika kupiga miayo ili kurekebisha joto lililozidi wakati huo.

Ubongo hufanya kazi kama kompyuta, ambayo hufanyakazi vizuri zaidi inapokuwa imepoa, hivyo maumbile ya kiasili hufanyakazi yake ya kujiendesha yenyewe pale kiungo chochote cha mwili kinapoonekana kuhitaji msaada.

Hata hivyo, utafiti mwingine unaonesha kwamba kupiga miayo kupita kiasi, kunaweza kuwa ni dalili ya tatizo lingine la kiafya, linalosababisha kuongezeka kwa joto kwenye ubongo au kuharibika kwa mfumo wa fahamu.

Kwa upande mwingine, kupiga miayo huwa ni dalili ya mabadiliko ya kimwili, kutoka hali ya uchangamfu kwenda uchovu au usingizi au kinyume chake. Kwa mujibu wa mwanasayansi wa Chuo Kikuu cha Maryland, Marekani, Dk. Robert Provineix, ni sawa pia kusema kuwa utafiti zaidi unahitajika ili kujua nini husababisha binadamu na wanyama wengine kupiga miayo.

Wakati mwingine, upigaji wa miayo mfululizo, huweza kuwa ni dalili ya matatizo ya moyo. Unapokutwa na hali kama hiyo mara kwa mara ni vyema ukaenda kuonana na daktari na kufanyiwa vipimo zaidi. 

Vile vile upigaji wa miayo mfululizo huweza kuwatokea wagonjwa wa kifafa, muda mfupi kabla ya kushikwa na kuanguka.Hivyo ni vyema kujitambua kama miayo unayopiga ni ya kawaida au siyo. Kwa sababu inawezekana kuwa ni dalili ya tatizo lingine kubwa la kiafya.  Ukatili wa kutisha kichanga chaokotwa kimekufa..!!

Matukio ya kinyama ya kuwatupa watoto hususani vichanga yameendelea kutokea katika maeneo mbali mbali hapa nchini Tanzania.
Jana katika mkoa wa Arusha eneo la  la Relin Themi Njiro, ameokotwa mtoto kichanga ambaye amepatikana akiwa tayari amefariki dunia baada ya kutupwa na mtua ambaye hajafahamika.

Akizungumza na kiwale11blog,diwani wa kata ya Themi venance kinabo,amesema bado haijajulikana mtu aliyemtupa kichanga huyo ametokea eneo gani.

Mtoto huyo amehifadhiwa katika Hospitali ya mkoa wa Arusha Mount meru huku  jeshi la polisi likiendelea na uchunguzi zaidi


Monday, 16 March 2015

Serikali kuifungia mitandao ya kijamii,Radio na TV zitakazofanya haya hapa..!!!

Mamlaka  ya Mawasiliano Tanzania  (TCRA), imesema iko mbioni kuifungia mitandao ya kijamii, redio na televisheni inayokiuka maadili ya Mtanzania.
Meneja Mawasiliano wa Mamlaka hiyo, Innocent Mungy, alisema kuwa mitandao hiyo ni pamoja na  facebook, whatsapp na  instagram.
Alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu changamoto zinazoikabili mamlaka hiyo kutokana na kuwapo kwa watumiaji wengi wa mitandao hiyo katika kuelekea Siku ya Mawasiliano duniani inayofanyika Machi 15, kila mwaka.
Mungy alisema kuwa Mamlaka hiyo inafanya utafiti ili kubaini mitandao inayoongoza kwa kulalamikiwa na wateja ili hatua zichukuliwe.

Aliwataka wamiliki wa mitandao kufuata maadili ikiwa ni pamoja na viongozi wa dini, wazazi, kuwafundisha wananchi na waumini wao kuwa na maadili ili kuondoa upotofu huo ambao unaweza kugeuza kizazi kisichofuata maadili na wengine kukosa ajira kutokana na kutumia mitandao vibaya.

Under 18 Uingereza kufunzwa Somo kuhusu ubakaji....

Wanafunzi kuanzia miaka 11 nchini Uingereza watafundishwa kuhusu tofauti kati ya ubakaji na tendo la ngono ambalo limetekelezwa kutokana na idhini ya wapenzi wawili kama mojawapo ya mipango ya kuwawapa ujuzi kuhusu maisha ya sasa nchini humo
Somo hilo ambalo litaanzishwa mara moja baada ya siku kuu ya Easter litaongezwa katika mtaala wa Uingereza baada ya wasiwasi kutolewa kwamba vijana walikuwa wakishinikizwa kushiriki katika ngono.
Nick Morgan ambaye ni katibu wa elimu alitoa tangazo hilo siku ya kimataifa ya wanawake.
''Lazima swala hili tulikabili kwamba mambo ambayo wasichana wetu wanapitia hayakuwepo wakati wa ujana weyu,kwa hivyo ni wajibu wetu kuhakikisha kuwa wasichana wetu wanamaliza shule wakiwa na uwezo wa kukabiliana na changaomoto watakazokumbana nazo wakiwa watu wazima'', aliandika.

Moto waunguza Hostel za Wasichana Mabibo Asubuhi hiiMoto ambao haujafahamika mara moja chanzo chake, umeteketeza baadhi ya mali za wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar Es Salaam wanaoishi katika Hostel za Mabibo.
Taarifa zinaeleza kwamba wanafunzi wakishirikiana na baadhi ya raia wamefanikiwa kuudhibiti moto huo, huku baadhi ya mali za wanafunzi wa kike katika hoteli hizo zikiteketea.
Hata hivyo wanafunzi hao waeelekeza lawama kwa kikosi cha zima moto ambao kinadaiwa kutofika kwa wakati.

unaweza msikia mmoja wa wanafunzi wanaokaa katika hostel hiyo akifunguka kuhusiana na moto huo,futa link hii

https://www.hulkshare.com/kiwamkali/mwanafunzi-mwingine

Mwanamke mwenye 'sura mbaya' atoa filamu..

Mwanamke anayedaiwa kuwa na sura mbaya duniani na mitandao inayomuonea ametoa filamu kuhusu maisha yake.
Maisha ya Lizzie Velasquez mwenye umri wa miaka 26 yalibadilika kabisa baada ya kuona kanda ya video katika mtandao wa tube iliodai kwamba yeye ndiye mwanamke mwenye sura mbaya duniani.
Lizzie ambaye alikuwa na miaka 17 wakati huo alikasirishwa kuona kwamba msichana aliyekuwa katika kanda hiyo ya video alikuwa yeye.
Kanda hiyo ilioonekana mara millioni 4 mtandaoni huku wengi wakiwacha ujumbe wa kuudhi kama vile ''angeuliwa alipozaliwa'',nilishangaa nilipoona ujumbe huo alisema Lizzie.

Ujumbe mwengine ulisoma ''kwa nini wazazi wake walimlea''.
Mwanamke huyo alipiga moyo konde na kuanza mtandao wake wa You Tube akiwaelezea watu kuhusu mwanamke huyo anayedaiwa kuwa mwenye sura mbaya zaidi.
Lizzie amesema kuwa anawasaidia wengine ambao wamekuwa wakionewa kuweza kupata msaada ama hata kupambana na maonevu hayo.
Mwanamke huyo pia anafanya kazi na Tina Meir ambaye mwana wao Mega alijiuwa baada ya kuonewa katika mtandao.

Saturday, 14 March 2015

Papa Francis atoa ishara za kujiuzulu.!!!!!

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis amedokeza kwamba huenda akafuata nyayo za mtangulizi wake Papa Benedict kwa kujiuzulu.
Akihojiwa na runinga moja ya nchini Mexico katika sherehe za maadhamisho yake ya pili tangu achaguliwe,Papa Francis amesema kuwa anahisi kwamba uongozi wake katika kanisa hilo hautaendelea kwa kipindi kirefu.
Amesema kuwa hatua ya Benedict kujiuzulu mwaka 2013 ni ya ujasiri na haifai kuchukuliwa kama ya kipekee.
Papa Benedict ndiye kiongozi wa kwanza wa kanisa hilo kujiuzulu tangu papa Gregory wa 12 mwaka 1415.
Papa Francis anasema kuwa anatamani maisha yake ya kuwa muhubiri na angependelea kuzuru maeneo kadhaa bila kujulikana.

Friday, 13 March 2015

Kesi ya rais wa Kenya yafungwa rasmi

Mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC imefunga kesi yake dhidi ya rais wa Kenya Uhuru Kenyatta .

Alikuwa ameshtakiwa na uhalifu dhidi ya binaadamu kufuatia ghasia zilizojiri baada ya uchaguzi wa mwaka 2007.

Wanawake wanaovaa nguo nyekundu huvutia Zaidii!!!

Wanawake wanaovalia mavazi ya rangi nyekundu,huwavutia sana wanaume ikilinganishwa na wale wanaovaa mavazi ya rangi nyengine. Kulingana na utafiti huo rangi hiyo huvutia sana na pia huwashirikisha wanawake wanaobeba laptopu nyekundu. Steven G Young wa chuo kikuu cha mji wa New York,aliandika katika jarida la maadili ya kisosholojia kuwa Ushahidi wa hivi karibuni unadai kwamba rangi husaidia katika kuwakutanisha watu wawili wanaopendana. Pia ameongeza kuwa raha inayopatikana miongoni mwa wanawake wakati wa tendo la ngono, hushirikishwa na wekundu wa mashavu,shingo na kifua. Wanawake wengi hupendelea kuvaa mavazi ya rangi nyekundu wakati wanapojiandaa kukutana na wanaume wanaowavutia. Ukilinganisha na rangi nyengine wanawake wanaovalia mavazi ya rangi nyekundu huvutia sana.

Idadi ya mimba za utotoni yaongezeka..!!!!!

Msichana mmoja kati ya wanne wenye umri wa miaka 15 hadi 19 ni mjamzito au ana mtoto imeelezwa. Idadi hii inawakilisha maisha halisi na kuonesha kwamba kama jitihada za makusudi hazitachukuliwa, wasichana wataendelea kukosa haki zao za msingi na kuzidi kuwa wategemezi. Hayo yalisema na mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akifungua mkutano wa kimataifa wa utafiti katika ukunga, ulioandaliwa na LUGINA Afrika Midwives Research Network (LAMRN) uliofanyika katika Hoteli ya Kunduchi jijini Dar es Salaam. Mama Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA),amesema vifo vya akinamama wajawazito na watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano,ni tatizo katika nchi zote zilizopo Kusini mwa Bara la Afrika hata hivyo jitihada mbalimbali zinafanyika ili kuhakikisha tatizo hilo linapungua au kumalizika kabisa. Kuhusu mimba za utotoni Mwenyekiti huyo wa WAMA, amesema tafiti zilizofanyika zinaonesha wasichana wanaanza kufanya mapenzi mapema zaidi wakiwa na umri mdogo, ukilinganisha na wavulana jambo linalopelekea kupata mimba za utotoni na hivyo kukosa elimu kwa kukatisha masomo yao

Mtoto akatwa uume kimakosa akitahiriwa...

Mtoto aitwaye Badru Muhidin mwenye umri wa miaka miwili, amepata pigo kubwa baada ya kukatwa uume wake kimakosa na babu yake aliyekuwa amempeleka kutahiriwa kienyeji huko Mbagala jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita. Mama mzazi wa mtoto huyo Mwajuma Hussein ambaye ni mkazi wa Yombo jijini Dar, amesema aliishi na mwanaye peke yake bila baba yake kwani walitengana Juni mwaka jana baada ya kuishi bila kufunga ndoa kwa muda mrefu, lakini mara kwa mara alikuwa akimpeleka mwanaye nyumbani kwa wazazi wa mumewe kuwasalimia. Amesema baada ya kumkuta katika hali hiyo, alianza kuhangaika naye hospitalini kutafuta msaada, alipofika Temeke aliambiwa na madaktari kwamba kijana wake alikatwa vibaya na hivyo analazimika kufanyiwa upasuaji ili kumnusuru. Babu wa mtoto huyo anashikiliwa na Jeshi la Polisi baada ya kufunguliwa shauri katika Kituo cha Polisi Mbagala Kizuiani kwa madai ya ukatili.