Wednesday 18 March 2015

Jimbo la Colorado lakusanya kodi ya Bangi zaid ya bil 24..l..



Kwa Tanzania Sheria zimebanwa zaidi kuzuia matumizi ya dawa za kulevya,lakini kwa Marekani wao kuna Majimbo ambayo yaliruhusu matumizi ya Bangi, uhalali huu umeingiza Bangi kuwa bidhaa halali kabisa kutumiwa na kuuzwa kama ilivyo bidhaa nyingine Majimbo kama ya Washington DC,Alaska na jimbo la colorado.
Story nyingine ni kwamba Jimbo la Colorado wamefanikiwa kukusanya kodi ambayo ni dola Mil. 15 (zaidi ya Bil. 27 Tshs).
Fungu hilo la kodi linapelekwa kujenga Shule mbalimbali kupitia mpango wa Jimbo hilo uliopewa jina la Building Excellent Schools Today (BEST)
Tangu kupitishwa utaratibu wa kuruhusu uuzaji wa bangi, unaambiwa maduka ya kuuza bidhaa hiyo rejareja mtaani kuanzia Jan. 1, 2014 mpaka sasa wamefanikiwa kukusanya kodi ambayo ni dola Mil. 15 ambazo zinasaidia kuboresha mazingira ya Shule za Umma katika Jimbo hilo.

0 comments:

Post a Comment