Tuesday 31 March 2015

Abiria aliandika barua kwa Rubani..!!!!!

Ishu ya ajali ya ndege ya Germanwings ambayo ilipata ajali katika milima ya Alps Ufaransa imekuwa ikizungumziwa sana hasa kutokana na ishu hiyo kuonekana kwamba rubani mmoja aliebaki ndani ya chumba cha marubani kuiangusha ndege hiyo kwa makusudi.
Watu wachache sana wanaweza kupakiwa kwenye Bodaboda, Bajaj, au gari halafu akishuka anamshukuru dereva kwa kumfikisha salama,watu wengi hawana utamaduni huo wa kushukuru.
Chukua hii inahusu barua ambayo imeandikwa na Bethanie ambaye alikuwa mmoja wa abiria aliyekuwa kwenye ndege, kamuandikia rubani Jai Dillon kumshukuru kwa kumfikisha salama.
Bethanie ameonesha pia kusikitishwa na tukio la ajali ya ndege ya Germanwings ambapo ndege hiyo ilikuwa na jumla ya watu 150.


0 comments:

Post a Comment