Monday 23 March 2015

Hizi hapa sababu 5 za Zitto Kujiunga ACT.!!!

Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe,ametaja sababu tano za kujiunga na chama cha ACT-Tanzania,huku akijigamba kuwa yeye ni mchapakazi na kwamba sasa mambo yote ni mbele kwa mbele.
Zitto ambaye aling’atuka kutoka kwenye nafasi ya Ubunge Ijumaa iliyopita kupitia Chadema na kujiunga na chama ACT siku moja baadae, amesema watu wengi wamekuwa wakijiuliza nini kingefuata baada ya ya kuachia nafasi. Zitto amesema anapenda kuwaarifu kuwa Machi 20, mwaka huu siku ya Jumamosi alijiunga na chama cha ACT na kukabidhiwa kadi namba 007194 ya uanachama na mwenyekiti ACT Tawi la Tegeta,na ameongeza kuwa amelipa ada ya uanachama hadi mwaka 2025. Zitto ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), alifunguka na kueleza sababu za kuhamia katika chama hicho ambacho hakina muda mrefu.
Msikie hapa chini Bwana Zitto Kabwe, alivyofunguka kuhusiana na uamuazi wake wa kuamua kujiunga na chama cha ACT.

0 comments:

Post a Comment