Monday 16 March 2015

Serikali kuifungia mitandao ya kijamii,Radio na TV zitakazofanya haya hapa..!!!

Mamlaka  ya Mawasiliano Tanzania  (TCRA), imesema iko mbioni kuifungia mitandao ya kijamii, redio na televisheni inayokiuka maadili ya Mtanzania.
Meneja Mawasiliano wa Mamlaka hiyo, Innocent Mungy, alisema kuwa mitandao hiyo ni pamoja na  facebook, whatsapp na  instagram.
Alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu changamoto zinazoikabili mamlaka hiyo kutokana na kuwapo kwa watumiaji wengi wa mitandao hiyo katika kuelekea Siku ya Mawasiliano duniani inayofanyika Machi 15, kila mwaka.
Mungy alisema kuwa Mamlaka hiyo inafanya utafiti ili kubaini mitandao inayoongoza kwa kulalamikiwa na wateja ili hatua zichukuliwe.

Aliwataka wamiliki wa mitandao kufuata maadili ikiwa ni pamoja na viongozi wa dini, wazazi, kuwafundisha wananchi na waumini wao kuwa na maadili ili kuondoa upotofu huo ambao unaweza kugeuza kizazi kisichofuata maadili na wengine kukosa ajira kutokana na kutumia mitandao vibaya.

0 comments:

Post a Comment