Tuesday 10 March 2015

LISSU ATANGAZA RASMI ZITTO SI MWANACHADEMA TENA

Mwanasheria mkuu wa chama cha upinzani nchini CHADEMA, Tundu Lissu leo ametangaza kuvuliwa uanachama kwa mbunge wa Kigoma Kasikani Zitto Kabwe baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaamkutupilia mbali pingamizi la mbunge huyo la kuzuia asijadiliwe. "Kwa mujibu wa katiba ya chama cha CHADEMA, mwanachama yoyote anapofungua kesi mahakamani dhidi ya chama chake, endapo atashindwa katika kesi hiyo atakuwa amejiondoa uanachama wake, kwahiyo natangaza rasmi rasmi Zitto Kabwe sio mwanachama tena wa Chadema. Kwa upande wake Zitto Kabwe amesema hawakuwa na wito wa mahakamani leo na Jaji wa kesi kahamishiwa Tabora na hawana taarifa ya Jaji Mpya, pia kaongeza kuwa Mwanasheria anafuatilia na atatoa statement. Licha ya kutupilia mbali kesi ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe, Mahakama kuu imemtaka kulipa gharama zote za kesi toka ilivyoanza. Mwaka jana Zitto Kabwe aliweka pingamizi mahakamni kuzuia kikao cha Kamati Kuu kumjadili na hoja yake ilikuwa ni kupinga kuitisha kamati kuu kabla shauri lake kusikilizwa na Baraza Kuu

0 comments:

Post a Comment