Saturday 7 March 2015

Wanawake wakulima wanaweza kutokomeza njaa

Wakati wa kuelekea siku ya wanawake duniani,viongozi wa Shirika la Chakula na Kilimo duniani(FAO),Mfuko wa Kimataifa wa Kilimo na Maendeleo(IFAD)na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani(WFP) wamekutana mjini Roma,Italia ili kusisitiza jukumu la wanawake wakulima katika kufanikisha usalama na uhakika wa chakula. Kwa mujibu wa mashirika hayo matatu ya kimataifa,kuwezesha wanawake wakulima na kufikia usawa wa kijinsia kunachangia kwa kiasi kikubwa katika kuimarisha usalama wa chakula na kupunguza umaskini vijijini. Akizungumza wakati wa mkutano huo mkuu wa IFAD Kanayo Nwanze,amesema nusu ya wakulima sasa ni wanawake wakati ambapo wanaume wanahamia mjini kutafuta riziki. Ameongeza kwamba ni lazima kutambua mchango wa wanawake ambao wanatekeleza kazi ngumu za kuvunja mgongo kwa ajili ya kulisha familia zao. Viongozi hao wamezingatia umuhimu wa kuwapatia wanawake fursa sawa za kufikisha bidhaa zao sokoni,kununua pembejeo na hatimaye kuwa na faida sawa kama wanaume.

0 comments:

Post a Comment