Jaribio la kwanza la ndege inayotumia umeme jua limefanyika leo baada ya ndege hiyo kufanikiwa kuanza kuruka asubuhi ya leo juma tatu tarehe 9/3/2015. Ndege hiyo iliruka majira ya saa 12 saa za Afrika Mashiriki ikianzia Abu Dhabi. Ndege hiyo yenye kiti kimoja ina mabawa yenye ukubwa wa jumbo jet huku ndege yenyewe ikiwa na uzito sawa na gari,mabawa yake yamefunikwa na vifaa vya kunasia mionzi ya jua yaani solar panels. Betri zake zina uwezo wa kuhifadhi nguvu ya umeme jua kutoka kwenye jua na hivyo kuiweza kusafiri hata nyakati za usiku. Marubani wawili wanaorusha ndege hiyo Bertrand Piccard na Andre Borschberg watapita katika hatua kumi na mbili za safari yao. Vipi ukipewa deal la kuruka na ndege hiyo nyakati za usiku tuuu ambapo jua halipo??
Kimataifa : EU na UNHCR Wasaini makubaliano ya zaidi bilioni 9 kuimarisha
Ulinzi na msaada wa wakimbizi
-
Mwandishi Wetu , Dar Es Salaam.
Umoja wa Ulaya (EU) na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi
Duniani (UNHCR) wamesaini makubaliano mapya ya u...
1 hour ago
0 comments:
Post a Comment