Monday 9 March 2015

Utafiti:Matumizi ya Paracetamol ni hatari kwa Afya..!!!

Matumizi ya kila siku ya dawa za kupunguza maumivu za paracetamol huongeza hatari ya ugonjwa wa moyo,kiharusi na kufupisha maisha ya binadamu, utafiti mpya umeonya. Paracetamol hupendelewa zaidi na madaktari wengi hudai zi salama kulinganisha na aspirin, ambayo imehusishwa na kuvuja damu tumboni na ibuprofen iliyohusishwa na magonjwa ya moyo na kiharusi. Lakini watafiti wa Uingereza waliofanya uchunguzi huo uliowahusisha wagonjwa 666,000 wanasema hatari iliyomo katika dawa hizo,huenda ilipuuzwa na sasa wameagiza uchunguzi ufanywe kuhusu usalama wake. Taarifa hizo iwapo ni za uhakika, itakuwa pigo kwa wengi kwa vile paracetamol zimezoeleka kuliko dawa nyingine yoyote ile ya kupunguza maumivu, na inapatikana kirahisi na kila mahali. Zaidi ya hayo makasha milioni 200 ya paracetamol huuzwa kila mwaka. Hata hivyo Prof. Philip Conaghan wa Taasisi ya Dawa ya Rheumatic and Musculoskeletal mjini Leeds Uingereza, amefichua kuwa matumizi ya muda mrefu ya paracetamol yana athari mbaya kiafya. Professa Conaghan alipitia tafiti nane zilizofanyika huko nyuma, kutathimini uhusiano baina ya matumizi ya muda mrefu ya paracetamol na matatizo ya kiafya kwa watu wazima.
Utafiti huo umebaini wagonjwa wanaopewa dawa hizo za kupunguza maumivu mwilini kwa muda mrefu,wana hatari kubwa ya asilimia 63 kufupisha maisha yao. Hatari ya kupatikana ugonjwa wa moyo na kiharusi iko juu kwa asilimia 68, huku pia kukiwa na hatari kubwa ya asilimia 50 ya kupatikana vidonda vya tumbo au hata kuvuja damu. Watafiti hao walihitimisha kuwa kutokana na ukubwa wa matumizi ya paracetamol na urahisi wa upatikanaji, uchunguzaji wa athari zinazoweza kupatikana kutokana na dawa hizo ulipuuzwa. Una maoni gani juu ya utafiti huu??

0 comments:

Post a Comment