Monday 23 March 2015

Lema asema Kinana amepigwa changa la macho Arusha.!!!




Siku moja baada ya Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana kuwapokea viongozi wawili akisema wanatoka Chadema na kumtuhumu Mbunge wa Arusha, Godbless Lema kuwa anatumia madaraka yake kujinufaisha na mali za umma, mbunge huyo amejibu akisema: “Kinana amepigwa changa la macho.”

Akiwa Arusha mwishoni mwa wiki Kinana aliwapokea waliokuwa wenyeviti wa Chadema katika Wilaya ya Monduli Amani Silanga na wa Ngorongoro Revocatus Palapala,lakini jana Lema amesema viongozi hao walikwishatimuliwa Chadema tangu mwaka 2013.
Akijibu tuhuma hizo Lema amesema Kinana amepigwa ‘changa la macho’ na amefanyiwa maigizo kama ya futuhi na watu wa usalama wameshindwa kumwambia ukweli.
Amesema mambo yote aliyoambiwa ni uongo mtupu ambao yeye hawezi kusumbuka nao.
Msikie hapa chini mheshimiwa Lema akitoa maelezo ya changa la macho alilopigwa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana.

0 comments:

Post a Comment