Wednesday 11 March 2015

Mh.Bendera aagiza uchunguzi kugundua chanzo cha moto kuunguza migodi Mererani

Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Manyara imetembelea katika migodi iliyoteketea kwa moto katika machimbo ya Tanzanite Mirereani Simanjiro huku mkuu wa mkoa huo Joel Bendera akiwaagiza wataalam wa Tanesco idara ya madini na jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa haraka kugundua chanzo cha moto huo ili hatua za kisheria zichukuliwe kwa watakao bainika. Katika ziara hiyo mkuu wa mkoa aliongozana na wataalam wa Tanesco idara ya madini na vyombo vya ulinzi na usalama ambapo kabla ya kuzungumza na wananchi alitoa nafasi kwa waathirika kutoa madukuduku yao nawo waliendelea kulalamikia uzembe uliyofanyika katika tukio ilo na kuendelea kusisitiza kuwa kuna hujuma katika tukio ilo na wengine wakilalamikia njaa na mazingira magumu ya kulala. Akitoa maelezo ya awali mkuu wa wilaya ya Simanjiro Mahamud Kambona ameeleza namna tukio ilo lilivyo waathiri wachimbaji wadogo na hatua za awali walizochukua. Ukafika wakati wa mkuu wa mkoa wa Manyara Dk Joel Bendera kutoa pole kwa niaba ya serikali na kuviagiza vyombo vinavyo husika kufanya uchunguzi wa kina kwa haraka ili kujuwa kama ilikuwa ni ajali ya kawaida au ni hujuma huku mkuu wa jeshi la polisi mkoa wa Manyara Christopher Fuime akitoa angalizo kwa wachimbaji wadogo kuhusu uhifadhi na matumizi ya mulipuko.

0 comments:

Post a Comment