Thursday 23 April 2015

Hawa ndio Marais Matajiri zaida Africa!!!

Jose Eduardo Dos Santos ndiye Rais anayeongoza kwa utajiri Afrika kutoka Angola, aliingia madarakani mwaka 1979, ana utajiri wa dola bilioni 20.

Wa pili ni Mohammed V1 Ni Mfalme wa Morocco ambaye amekaa madarakani kwa miaka 15, ana utajiri wa dola bilioni 2.
Wa tatu ni Teodoro Obiang Nguema Mbasogo: Rais huyu wa Equatorial Guinea aliingia madarakani 1979, ana una utajiri wa dola milioni 600 licha ya wananchi wa nchi hiyo kuishi maisha ya kimaskini kutokana na uchumi wao kuwa chini.
Wa nne ni Uhuru Kenyatta ni Rais wa Kenya ambaye alichaguliwa mwaka 2011, ana utajiri wa dola milioni 500, mbali ya kuongoza nchi ana vyanzo mbalimbali vya utajiri ikiwa kuwa na hisa nyingi katika kampuni mbalimbali,benki na mahoteli makubwa ya kifahari.
Wa tano Paul Biya ni Rais wa Cameroon tangu mwaka 1982, ana utajiri wa dola milioni 200, unaambiwa ndiye rais anayetumia kiasi kikubwa cha pesa katika ziara zake kuliko marais wote duniani na hutumia euro 30,000 kwa siku katika ziara zake.
Wa Sita ni King Mswat iii Ni mfalwe wa Swazland akiwa na utajiri wa dola milioni 100, anashika nafasi ya 15 katika familia za kifalme tajiri duniani, Unaambiwa wake zake 13 hutumia zaidi ya dola milioni sita kufanya manunuzi yao pekee, pia Serikali yake hutenga bajeti ya dola milioni 61 kila mwaka kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.
Wa saba ni Idriss Derby Ni Raisi wa Chad tangu mwaka 1990 na ana utajiri zaidi ya dola milioni 50.
Wa nane ni Robert Mugabe wa Zimbabwe, ana zaidi ya miaka 26 akitawala nchi ya Zimbabwe, utajiri wake ni dola milioni 10.








0 comments:

Post a Comment