Tuesday 21 April 2015

Wafugaji hatutahiminiwi: Watu wa asili..!!!

Mwakilishi wa jamii ya asili ya wafugaji iitwayo Samburu kutoka Kenya ambaye pia anawakilisha
mfuko wa wanawake wa jamii hiyo, Samburu Women Trust, Jane Meriwas amesema ni muhimu jamii ya kimataifa na kitaifa itambue haki za wafugaji na kuipa fursa jamii hiyo ambayo inaishi kwa kuhamahama kutokana na kutafuta malisho.
Katika mahojiano na idhaa ya kuswahili ya radio Un mjini New York anakohudhuria kongamano la 14 la watu wa asili Bi Meriwasi amesema jamii za wafugaji nchini Kenya zimeathiriwa na mambo mengi ikiwamo mabadiliko ya tabia nchi.
Bonyeza hapa chini kusikiliza mahojiano aliyofanya na  mtangazaji wa idhaa hiyo.



0 comments:

Post a Comment