Thursday 9 April 2015

Story hot Magazetin Leo April 9 2015


Hizi ndizo story Hot ambazo Editors wa magazeti mengi ya leo wameona zina uzito wa wewe kuzisoma katika magazeti ya leo mimi nakuwekea hapa kwa ufupi tu.
Kiongozi wa Chama cha ACT, Zitto Kabwe
amesema zaidi ya Wabunge 50, watajiunga na chama hicho, Wizara ya kilimo na chakula imewasimashisha kazi wakurugenzi watatu kwa kukutwa na tuhuma mbalimbali,TAKUKURU imewataka wananchi kuwachagua viongozi waadilifu wasiojihusisha na rushwa, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Harrison Mwakyembe amesema jamii za Afrika zinatakiwa kuwa kitu kimoja ili kuepuka machafuko yanayotokea.
Jeshi la Polisi limetoa onyo kwa wafuasi wanaotaka kumsindikiza Askofu Gwajima kwenda kuhojiwa,TABOA imesema madereva waliopanga kugoma hawatambuliwi kisheria, Serikali inatarajia kuzibana taasisi za kibiashara ili kujiunga na soko la hisa ili ziweze kufanya shughuli zake kwa uwazi, na wazazi wa Mtanzania, Rashid Charles Mberesero anaetuhumiwa kuhusika katika mauaji katika Chuo cha Garissa Kenya, wameelezea kushtushwa na taarifa za mtoto wao.


0 comments:

Post a Comment