Tuesday 21 April 2015

Habari Gumzo kwenye Magazeti leo April 21 2015



Moja wapo ni hii ya inayosema ‘CHADEMA, ACT jino kwa jino’, wanazidi kuchuana kwenye mikutano huku viongozi wake wakishutumiana, iko iliyoandikwa kuhusu wakazi wa Hanang’ Manyara kutangaza kumuunga mkono Wakili Duncan Mayomba akigombea Ubunge kwa kuwa amekuwa akiwatetea sana wakazi wa Wilaya hiyo kwenye masuala ya Kisheria.
Afande Sele kaandikwa nae, amesema anataka kuwa Mbunge wa tofauti na sio Ubunge wa kuvaa suti na kupokea Rushwa.
Chuo cha UDSM kimeshika nafasi ya kumi kwa ubora Afrika, Serikali imetangaza kuzifuta taasisi zaidi ya elfu kumi za kidini na NGO ambazo zimetajwa kuvunja kanuni mbalimbali ikiwemo kujihusisha na siasa.
Headline nyingine ni ishu ya NEC kutangaza kuwasili mashine mpya za BVR kwa ajili ya kuandikisha Wapigakura TZ ndani ya wiki hii, nyingine ni kuhusu Serikali kutangaza kuwarudisha TZ watu wote walio tayari kurudi kutoka Afrika Kusini.

0 comments:

Post a Comment