Tuesday 14 April 2015

HIZO NDIO ZIPO MBELE SANA KWENYE MAGAZETI YA LEO APRIL13 2015


Nimekutupia hapa kiduchuu tuu,habari ambazo zipo katika magazeti mengi ya leo April 14-2015
Miili 19 ya watu walioteketea kwa moto katika ajali ya basi na lori Morogoro, imezikwa katika kaburi la pamoja
Kilosa, Wasomi na wanasiasa wamesema nchi inapita katika kipindi kigumu kwa sasa kulingana na matukio mbalimbali yanayotokea, Serikali imeshindwa kuweka wazi kufungwa kwa shule zake za sekondari kutokana na ukosefu wa chakula, ndoa ya mwanamke mwenye miaka 54 na kijana wa miaka 25 yakwama Dar, Rais Kikwete amesema bado hajapelekewa majina ya watu 16 waliohukumiwa kifo kutokana na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif jana alifika mahakama ya Kisutu kusikiliza kesi ya wafuasi wa chama cha CUF, Serikali imetangaza rasmi ukumbi wa Nkrumah wa Chuo Kikuu Dar na meli ya Mv Liemba kuwa sehemu ya urithi wa taifa, Jeshi la Polisi Katavi linamshikilia mganga wa jadi kwa tuhuma za kukutwa na fuvu la kichwa cha binadamu na BAWATA imepiga marufuku baadhi ya waganga wanaotoa huduma kwenye nyumba za wageni.

0 comments:

Post a Comment