Tuesday 7 April 2015

Leo ni Karume Day..!!Unajua aliyofanya Rais Huyu





Kila Aprili 7 Watanzania tunakumbuka kifo cha aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Abeid Amani Karume aliyeuawa kwa kupigwa risasi tarehe
kama ya leo mwaka 1972.
Miaka zaidi ya 40 iliyopita hapo tarehe 7 Aprili 1972 Rais wa kwanza wa Zanzibar Sheikh Abeid Amani Karume, aliuwawa kwa kupigwa risasi katika jengo la Makao Makuu ya Chama cha Afro-Shirazi huko Kisiwandui mjini Zanzibar.

Rais Abeid Amani Karume muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar,alizaliwa katika kitongoji cha Pongwe, Mudiria ya Mwera kisiwani Unguja tarehe 4 Agosti 1905.

Karume ni mtoto wa kwanza kuzaliwa katika familia ya watoto watano ya Bwana Amani Karume na Bibi Amina binti Kadir (Amina Kadudu).

Wakati wa matayarisho ya Mapinduzi ya 1964 Abeid Karume alikuwa mwenyekiti wa kamati ya watu kumi na nne walotayarisha Mapinduzi hayo kwa siri.

Akiwa na umri wa miaka 59 Karume aliongoza Mapinduzi ya 1964 Zanzibar, na alitangazwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na vilevile kubaki na wadhifa wake wa Rais wa Afro- Shirazi Party.

Kwa vyovyote vile jina la Abeid Karume halitosahaulika katika historia ya ukombozi wa Zanzibar.

Katika kumbukumbu ya siku hii ya Rais Abeid Amani Karume, nimezungumza na naibu katibu mkuu wa chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA visiwani zanzibara bwana Salum Mwalimu.

Na kwanza nikamuuliza je Wazanzbari na watanzania kwa ujumla, tunamuenzi Rais Karume kwa jinsi inavyostahili
(kiwa interview with Salum Mwalimu.)





0 comments:

Post a Comment