Timu nne zimetinga hatua ya nusu fainali katika ligi ya mabingwa barani
Ulaya iliyokamilika hapo jana, baada ya Real Madrid ya Hispania na
Juventus ya Uitaliano kufanikiwa kuingia nusu fainali.
|
Javier Hernandez akishangilia goli mbele ya mashabiki wa Real Madrid
|
Wakicheza katika uwanja wao wa nyumbani wa Santiago Bernabeu, Madrid
walilazimika kusubiri hadi dakika ya 88, walipopata bao lao la pekee
lililotiwa kimia Javier Hernandez almaarufu kama Chicharito, na hivyo
kuhitimisha safari ya Atletico Madrid.
Katika msimu uliopita huko Lisbon Ureno, Atletico walitolewa na Real Madrid katika hatua ya fainali.
|
Timu ya Juventus
|
Nayo
Juventus imezima matumaini ya Monaco ya Ufaransa kwa kulinda bao lake
lililofungwa katika mechi ya awali na hapo matokeo ikawa sare ya bila
kutofungana.
Hata hivyo nyota ni njema kwa Spain ambao sasa
wanawakilishwa na timu mbili ambazo ni Real Madrid na Barcelona.
0 comments:
Post a Comment