Monday, 20 April 2015

Mfalme Zwelithini kutuliza raia Afrika Kusini!!!!


Goodwill Zwelithini, Mflame wa Zulu
 Mfalme wa Jamii wa Wazulu nchini Afrika Kusini, Goodwill Zwelithini, anatarajiwa kutoa wito kwa raia wa nchi hiyo kujiepusha na ghasia, kufuatia kuongezeka kwa mashambulio ya kibaguzi nchini humo.

Mfalme huyo ameshutumiwa kwa kuchochea mashambulio hayo ambayo yamesababisha vifo vya watu saba.
Zwelithini, alinukuliwa akisema kuwa raia wote wa kigeni wanapaswa kurejea katika mataifa yao.
Zaidi ya watu mia tatu wamekamatwa kuhusiana ghasia hizo.
Maelfu ya watu wanatarajiwa kufurika uwanja mmoja ulioko mji wa Mashariki wa Durban kusikiliza hotuba hiyo ya Mfalme Zwelithini.
Amekariri kuwa matamshi yake hayakufahamika.
Miongoni mwa washukiwa waliokamatwa hivi karibuni na wanaume watatu ambao wanatuhumiwa kuhusika na mauaji ya rais mmoja wa Mozambique katika eneo la Alexandra viungani mwa mji mkuu wa Johannesburg.
Picha kadhaa zimeonyesha Emmanuel Sithole akindungwa kisu huku umati mkubwa ukitizama.
Mama mmoja raia wa kigeni ambaye nyumba yake ilivamiwa nchini Afrika Kusini
Rais wa nchi hiyo Jacob Zuma, amesema mashambulio hayo yanakwenda kinyume na maadili yote wanayoamini.
Makundi kadhaa yaliyojihami yameshambulia na kupora maduka kadhaa yanayomilikiwa na wahamiaji kutoka mataifa mengine ya Afrika.
Huku idadi ya watu wasio na kazi nchini humo, ikikadiriwa kuwa zaidi ya asilimia Ishirini na nne, raia wengi wa taifa hilo wamewashutumu raia wa kigeni kwa kuchukua nafasi zao za kazi.
Maelfu ya raia hao wa kigeni, wamekimbia makwao na sasa wanaishi katika kambi za muda, ili hali mataifa jirani wameanza shughuli ya kuwahamisha raia wao.
Siku ya Jumapili, serikali ya Zimbabwe imetuma mabasi kadhaa mjini Durban kwenda kuwachukua raia wake wapatao mia nne.
Takwimu rasmi za serikali zinakadiria kuwa kuna raia milioni mbili wa kigeni wanaoishi nchini Afrika Kusini, lakini wengi wanahoji kuwa idadi hiyo huenda ni kubwa zaidiVia>>BBC

Related Posts:

  • Sherehe za nyama ya mbwa zaanza Uchina….! Sherehe ya kula nyama ya mbwa kusini magharibi mwa China,imeanza huku kukiwa na pingamizi miongoni mwa wanaharakati wa haki za wanyama. Takriban mbwa 10,000 watachinjwa na nyama yao kuliwa katika sherehe hizo,zitakazofany… Read More
  • Mazungumzo ya amani Burundi kuanza tena… Rais Pierre Nkurunziza Mazungumzo ya kutafuta amani nchini Burundi, yanatarajiwa kuanza tena leo baada ya kusitishwa kwa siku kadhaa. Mazungumzo hayo ni kati ya serikali, vyama vya upinzani na makundi ya kutetea haki za … Read More
  • Mwalimu mkuu ashiriki ngono na wanafunzi……!! Mwalimu mmoja mkuu, amekiri kufanya ngono na wavulana wawili wenye umri mdogo. Anne Lakey mwenye umri wa miaka 55 kutoka eneo la Stanley katika kaunti ya Durham, amekanusha makosa 13 dhidi yake ya kufanya matendo ya aibu … Read More
  • Zaidi ya watu mil 1 wanatumia dawa za kulevya China..! China ni nchi ambayo adhabu zake kwa wahusika wa dawa za kulevya hazina salia mtume kabisa yaani ukishikwa basi adhabu ya kifo inachukuwa hatamu. China wana sheria kali sana dhidi ya wahusika wa dawa za kulevya, ila st… Read More
  • Wanaovalia suruali za kubana waonywa… Suruali ndefu aina ya jinsi zinazobana, zinaweza kusababisha madhara makubwa kwa mishipa na misuli, madaktari wameonya. Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 35,alilazimika kutolewa ndani ya suruali ndefu aina ya Jeans b… Read More

0 comments:

Post a Comment