Ray
Tomlinson raia wa Marekani ambaye ndiye aliyevumbua utumaji wa barua pepe, kwa
Kiingereza e-mail amefariki dunia.
Tomlinson amefariki akiwa na umri
wa miaka 74.
Mgunduzi huyu aliibuka na wazo la
kutuma ujumbe wa kieletroniki, kutoka mtu mmoja hadi mwingine kupitia mitandao
mbali mbali mwaka 1971.
Aliandika ujumbe wa kwanza wa
barua pepe wakati akifanya kazi Boston, kama Mhandisi wa kompyuta.
Pia alikuwa mwanzilishi wa
matumizi ya alama "at"(@) kuwa ndio alama kuu ya utumaji wa barua
pepe.
Wakati wa uhai wake Tomlinson
alisema hawezi kukumbuka barua pepe yake ya kwanza ilielezea nini.
0 comments:
Post a Comment