Mahakama
katika mji mkuu wa India imeamua kwamba ni kosa, kwa mke kumuita mumewe Tembo
na kosa hilo linaweza kuwa sababu ya kupewa talaka.
Mahakama Kuu mjini Delhi imeidhinisha uamuzi wa mahakama ya
chini hiyo, uliotolewa mwaka 2012 ambao uliidhinisha talaka kwa mke
atakayemwita mumewe jina hilo.
Mahakama hiyo ilisema mtu kumuita mumewe Tembo ni kumtendea
ukatili wa kiakili.
Mfanyabiashara aliyeitwa ndovu na mkewe ana umri wa miaka 35,
na alikuwa na uzani wa kilo 100.
Amesema mkewe alizoea kumuaibisha kwa kuwa ni mnene na kutoweza
kutimiza haja yake ya kimapenzi, vyombo vya habari India vimeripoti.
Mwanamke huyo alikuwa ameiambia mahakama hiyo kwamba, madai
ya mumewe hayakuwa na msingi lakini mahakama haikukubaliana naye.
0 comments:
Post a Comment