Tuesday 29 March 2016

NDEGE YA MISRI ILIYOTEKWA YATUA CYPRUS….

Ndege iliotekwa nyara imetua katika uwanja wa ndege wa Larnaca nchini Cyprus.

Duru kutoka kwenye ndege hiyo pamoja na za serikali ya Misri zimenukuliwa zikisema kuwa, ndege hiyo ya abiria iliyokuwa ikisafiri kutoka mjini Alexandria kuelekea Cairo ilitekwa nyara na watu waliojihami.
Waliiamrisha ndege hiyo kutua Cyprus, msemaji wa shirika la ndege la EgyptAir alinukuliwa akisema.
Shrika la habari la Cyprus limeripoti kwamba watu 55 wamo ndani ya ndege hiyo.
Kulikuwa na ripoti za awali kwamba zaidi ya watu 80 wamo ndani ya ndege hiyo.
Ndege hiyo aina ya MS181 Airbus A320, ilibeba abiria 81 taarifa za awali zilisema.
Abiria aliyedaiwa kuwa alikuwa amevaa ukanda wa mlipuaji wa kujitolea mhanga, aliagiza rubani kuelekea Cyprus kulingana na EgyptAir.
Maafisa wa polisi wa Cyprus wamesema kuwa wale walioiteka hawakuitisha chochote ilipotua.

Uwanja wa ndege wa Larnaca umefungwa, huku ndege zilizosubiriwa kutua zikielekezwa kwingineko.

0 comments:

Post a Comment