Tuesday 1 March 2016

WANAOISHI KATIKA MAPIPA YA TAKA UK WAONGEZEKA…

Idadi ya watu wasio na makao na ambao sasa wanaishi katika mapipa ya taka, inaendelea kuongezeka nchini Uingereza, kulingana na kampuni kubwa ya kuzoa takataka nchini humo.

George ni miongoni mwa idadi kubwa ya raia nchini Uingereza aliyepatikana akilala katika mapipa ya takata kulingana na kampuni hiyo ya kuzoa taka ya Biffa.
George amekuwa bila makao tangu alipopoteza kazi yake ya uhandisi kabla ya krisimasi, mwaka jana na kumfanya kushindwa kulipa kodi ya nyumba.
Mnamo mwaka 2014 kampuni hiyo iligundua watu 31 waliokuwa wakilala katika mapipa tofauti ya takataka.

Mwaka mmoja baadaye idadi hiyo iliongezeka na kufikia 93, na mwaka huu ambao unaisha mwezi Machi idadi hiyo imefikia 175 kufikia sasa.

0 comments:

Post a Comment