Thursday 10 March 2016

ATUNGWA MIMBA YA PACHA NA WANAUME WAWILI…...!

Mapacha wa kipekee wamezaliwa nchini Vietnam, baada ya kugundulika kuwa walitungwa na baba wawili tofauti.

Taarifa zinasema familia za mapacha hao iligundua kuwa watoto hawakufanana hata kidogo, hivyo ikawalazimu kufanyiwa uchunguzi wa celi za DNA.
Mbivu na mbichi zilipobainika watoto hao waligundulika kuwa hawana uhusiano wa aina yeyote.
Taasisi ya utafiti wa maumbile Genetic Association, inasema hali kama hii hufanyika japo siyo kawaida.
Mwanamke anaweza kupata mapacha na baba wawili tofauti, ikiwa atajamiana na wanaume wawili katika kipindi cha siku chache wakati ambapo mayai yake yameiva.
Kulingana na profesa Dinh Luong mtafiti mkuu wa taasisi ya utafiti wa seli na jeni nchini Vietnam, matokeo ya uchunguzi wa jeni ulibaini asilimia 100% kuwa watoto hao hawakuwa wa baba mmoja.
Kuna visa 10 pekee vya mapacha waliozaliwa na baba tofauti duniani, huenda kuna hali kama hiyo lakini pengine wazazi huwa hawaelewi imesema taasisi hiyo.

Vyombo vya habari vya Vietnam vilianza kuripoti kuhusu mapacha hao, baada ya mmoja wa jamaa wao kusema pacha mmoja hakufanana kabisa na mwenzake pia na wakiwemo wazazi.

0 comments:

Post a Comment