Kiongozi
wa kidini wa mtandao wa kigaidi wa Al Qaeda Osama Bin Laden aliacha urathi wa
dola milioni 29 kufadhili Jihad alipouawa mwaka 2011.
Hayo ni kwa mujibu wa wasia wake
iliofichuliwa leo.
Aliihimiza familia yake kuheshimu
waysia wake na kuwashauri ''watumie mali yake yote kuendeleza jihad''
Mali yake na wasia wake ni
miongoni mwa maelfu ya stakabadhi muhimu zilizofichuliwa hii leo na maafisa wa
Marekani.
Aidha Bin Laden alimtaka babake
amtunzie mke na wanawe endapo ataaga dunia.
Kiongozi huyo wa mtandao wa
kijihad wa Al Qaeda aliuawa na majeshi ya Marekani mwaka wa 2011 katika
shambulizi la kufumania lililotekelezwa ndani ya Pakistan.
0 comments:
Post a Comment