Thursday, 17 March 2016

TRUMP ASEMA HUENDA FUJO ZIKAZUKA MAREKANI…

Mfanyabiashara tajiri Marekani Donald Trump, amesema anafikiri kutatokea fujo iwapo ataongoza kwa wajumbe kisha chama chake cha Republican kitakosa kumuidhinisha awanie urais.

Bw Trump alishinda mchujo katika majimbo matatu zaidi,likiwemo jimbo la Florida mnamo Jumanne, ingawa alishindwa katika jimbo jingine muhimu la Ohio.
Hatua yake ya kushindwa Ohio huenda ikawawezesha wahafidhina wadhibiti wa chama cha Republican ambao hawajafurahishwa na mtazamo wake, kumpendekeza mgombea mwingine kwenye mkutano mkuu wa kuidhinisha wagombea Julai.
Hayo yakijiri Bw Trump amesema hatashiriki mdahalo katika runinga ya Fox News wiki ijayo akisema ametosheka na midahalo.

Katika chama cha Democratic Hillary Clinton ameimarisha uongozi wake na kumshinda mpinzani wake wa pekee Bernie Sanders, katika majimbo manne yaliyofanya mchujo Jumanne.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment