Thursday, 10 March 2016

APATIKANA NA HATIA YA KUMUIBA MTOTO…!!

Mahakama kuu mjini Cape Town nchini Afrika Kusini, imempata na hatia mwanamke mmoja kwa kumteka nyara mtoto mchanga kutoka hospitali moja karibu miaka 20 iliyopita.

Mtoto huyo anadaiwa kunyakuliwa kutoka Katika kitanda cha mama yake, siku tatu baada ya kuzaliwa mnamo mwaka 1997.
Mwaka uliopita mtoto huyo aliunganishwa tena na familia yake, baada ya kujenga urafiki na msichana mdogo katika shule yao ambaye walifanana sana.
Uchunguzi wa DNA ulithibitisha kuwa wasichana hao walikuwa ni dada wawili.

Mwanamke anayeshutumiwa amekanusha kuhusika, akisema kuwa alipewa mtoto na mtu mwingine baada ya kupoteza mimba.

Related Posts:

  • NASA wapata taarifa za Sayari ya Pluto…… Wana sayansi wa NASA kutoka Marekani wanasema kuwa,majaribio yao ya kurusha chombo kwenda katika sayari ya Pluto yamekuwa na mafanikio makubwa. Chombo hicho kimefanikiwa kutuma taarifa katika kituo cha utafiti huo cha Ma… Read More
  • Polisi 4 wauawa katika shambulizi Dar.... Maafisa wanne wa polisi na raia wawili wameuawa baada ya watu wasiojulikana kuvamia kituo cha polisi mjini Dar es salaam Tanzania. Shambulizi hilo limetokea katika kituo cha polisi kilichoko Ukonga, viungani mwa jiji kuu l… Read More
  • Michuano ya Kagame kuanza kutimua vumbi...!!! Michuano ya klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati jumamosi wiki hii inaanza kutimua vumbi mjini Dar es Salaam Tanzania huku jumla ya vilabu 13 vikishiriki. Rais wa Rwanda Paul Kagame anatarajiwa kutoa kiasi cha dola el… Read More
  • Msako mkali Mexico wa muuza mihadarati…… Gwiji la Mihadarati anayesakwa Mexico Joaguin Guzman Mamlaka ya nchini Mexico limeanza msako mkali wa kumtafuta Joaguin Guzman gwiji la biashara ya madawa ya kulevya duniani, kufuatia kutoroka kwake katika gereza lenye u… Read More
  • Kambi ya jeshi yaporomoka na kuua 23 Urusi… Takriban wanajeshi 23 wa Urusi wameuawa karibu na mji wa Omsk ulioko Siberia,baada ya jengo la kambi ya kijeshi kuporomoka. Wanajeshi wengine 19 waliokolewa kutoka kwa vifusi vya jengo hilo. Mwanajeshi mmoja aliyeokolew… Read More

0 comments:

Post a Comment